KAMATI KUU YA NLD KUKUTANA KESHO
Kamati Kuu ya Chama cha National League for Democracy (NLD),
Itakutana kesho Jumapili, tarehe 23 Februari 2025, saa 6:00 mchana,
Mahali, Popex Hotel Buguruni shell, Jijini Dar es Salaam.
Agenda za Kikao:
1. Kutathmini hali ya kisiasa nchini baada ya uchaguzi.
2. Kutathmini kwa kina uhai wa chama nchini, baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji.
3. Maandalizi ya Halmashauri Kuu kwa ajili ya kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa.
4. Kuandaa na kupanga ratiba ya kuchagua wagombea wa nafasi mbalimbali za uwakilishi ndani ya chama, ikiwemo nafasi za udiwani, ubunge, na urais wa Zanzibar, na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
5. Kujadili amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
6. Na, mengineyo.
Imetolewa na:
Ofisi ya Katibu Mkuu
Makao Makuu.
Tandika, Jijini, Dar es Salaam.
Mhe. Sabra Anthony Masanza, Katibu wa Katibu Mkuu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni