DIWANI LYOTO AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI ILANI UCHAGUZI CCM.
Na Mussa Augustine.
Diwani wa Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Manfredy Lyoto amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kata ya Mzimuni kwa muda wa miaka mitano 2020/2025
Taarifa hiyo imewasilishwa februari 22,2025 ,na inahusu utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na utatuzi wa changamoto katika sekta ya Elimu,Afya,Miundombinu,Fursa za Ajira,Maendeleo ya Jamii,utawala Bora na Madaraka kwa Wananchi,Mahusiano ya CCM na Serikali,pamoja na Michezo.
Akizungumza na Waandishi wa habari kando ya Mkutano Mkuu Maalumu wa kuwasilisha taarifa hiyo kwa wanachama wa CCM kata ya Mzimuni uliyofanyika Magomeni Jijini Dar es salaam ,Diwani Lyoto amesema kwamba kwenye uongozi wake wa miaka mitano ameweka kipaumbele zaidi kwenye Elimu.
"Sababu umuhimu wa Elimu naujua,bahati nzuri mimi mwenyewe nimesoma,nimesoma wakati enzi za Mwalimu ambapo tulikua tunalipiwa kila kitu,wazazi walikua wananunua sare tu za shule lakini mahitaji mengine kama vile chakula hadi sabuni za kufulia tulikua tunapewa na Serikali." amesema Lyoto
Amendelea kusema kuwa Nchi yoyote Duniani iliyowekeza vizuri kwenye Elimu lazima inaendelea,hivyo Elimu ndio mwarobaini wa maendeleo hakuna kitu kingine.
Amesema kwamba pamoja na Elimu kuipa kipaumbele ,pia kuna vipaumbele vingine ambavyo atavizingatia ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara kwani barabarani za kata ya Mzimuni bado ni mbovu.
"Nataka tuje tuzitazamie kwa bajeti ya Manispaa,bajeti ya Serikali kuu,pia nitakuja na mbinu zangu binafsi,sababu nafahamiana na wawekezaji wengi nitawaomba wanisaidie kujenga kilometa kadhaa za barabara ndani ya kata yangu ya Mzimuni,na Mimi wananiheshimu na wananiamini nauhakika hilo litafanikiwa.
Aidha Diwani Lyoto amesema kuwa amefanikiwa kwa kiasi kukubwa kutatua kero zilizokua zikiwakumba wananchi wa Kata hiyo kutokana na kushirikiana vyema na Wananchi kwa kuwashirikisha katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Aidha amesema kwamba kila kitu kitakua rahisi na kiongozi utakua unawangalia watu zaidi kuliko wewe mwenyewe.
Aidha Lyoto ametoa wito kwa Wanachama wa CCM kuwangalia na kuwachunguza watu wanaotoa hongo kwa ajili ya kuwachagua kwenye nafasi za uongozi kwani wengi wao hawana mapenzi ya dhati na Wananchi bali wanajali maslahi yao binafsi.
"Kuna wakati kwenye chama kuna makosa yanafanyika watu hawangalii na hawamchunguzi mgombea,wengi wanangalia ametoa nini,na mtu akitoa nini maanayake kuna kitu amenunua,na ukishakinunua mhusika hakudai tena,wewe unaendelea kuwa kiongozi lakini hauwajibiki kwao kwasababu ulijiweka mwenyewe madarakani sio wao walikuweka"amesema
Nakuongeza kuwa "watu wetu kiukweli wanahitaji huduma nzuri kutoka kwa viongozi wao,kuna sehemu ukifika kwa sisi ambao machozi yetu yapo karibu unaanza kudondosha machozi unapomuona Mwananchi yupo katika shida,mtu anakuja Ofisini kwangu,
anasema mheshimiwa diwani ninasiku tatu sijala,ukimuliza anakuambia kweli hatuna kitu chochote,sasa akinikuta mfukoni sina kitu lakini nahitaji kumsaidia naishia kudondosha machozi pamoja na yeye,kwahiyo uongozi unahitaji mapenzi ya dhati na utu kwa wale unaowaongoza.
Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama akiwemo Mbunge wa Kinondoni(CCM) Tarimba Abas, Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dar es salaam Ally Bananga pamoja Mwenyekiti CCM Wilaya ya Kinondoni Shaweji Mkumbula.
DIWANI LYOTO AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI ILANI UCHAGUZI CCM.
Reviewed by mashala
on
09:39:00
Rating: 5

Hakuna maoni
Chapisha Maoni