CCM yaishika pabaya ACT Zanzibar
Chama Ca Mapinduzi (CCM) kimemshangaa Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo , Ismail Jussa Ladhu , kwa kukosa vipimo na maarifa ya kisiasa huku akiendelea kuwadangaya wananchi kwa kuponda Maendeleo yalioletwa na SMZ
CCM kimemtaka Jussa kutozichezea akili za wazanzibari kwani maendeleo anayoyaponda yako sanjari na ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi ya ACT mwaka 2020/2025.
Siri hiyo imefichuliwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis , aliyesema baadhi ya ahadi zilizotekelezwa na SMZ chini ya Rais Dk Huseein Mwinyi , zimo katika Ilani ya ACT Wazalendo .
Mbeto akionyesha kumshangaa Jussa ,alisema yalioahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2020- 2025, yanafanana na ahadi za ACT, hivyo ni kituko kumsikia Jussa akibeza ujenzi wa shule za Maghorofa.
Akitoa mfano , alisema katika kifungu cha 4.3 kuhusu Michezo, Sanaa na Burudani , ukurasa wa 39, ilani ya ACT, kama kingeingia ikulu , kiliahidi kuimarisha maeneo ya mapumziko kwa kushiriana na vikundi vya Wanawake na Vjana ili kuongeza ajira.
Pia Mbeto alikitaja kifungu cha 3.2.1 cha ilani ya ACT, imeahidi endapo kingeshinda uchaguzi , kingeboresha Miundombinu ya huduma za Afya kwa kujenga Zahanati ,Vituo vya Afya na kuzijengea uwezo hospitali za Wilaya na Mikoa.
"Nimewahi kusema mahali fulani Jussa kifikra na kiitikadi hana tofauti na kibaraka wa zamani huko Zimbabwe Ian Douglas Smith .Kazi yake kubwa ni kupinga mema yote ya kimaendeleo kwa Afrika na watu wake "Alieleza Mbeto
Katibu huyo Mwenezi , alisema juhudi za kimkakati na kisera zilizofanywa na Serikali ya Rais Dk Mwinyi kupitia ilani ya CCM mwaka 2020 - 2025, ametekeleza kwa ufanisi mkubwa sekta za Elimu, Uwekezaji, utalii Michezo ,Sanaa na Afya ,tena kwa kiwango cha juu.
"Jussa na ACT msiwafanye wananchi wa Zanzibar hawajui malengo yenu . Mmeshindwa kutekeleza mradi wenu wa siri acheni kuburuza wananchi .Rasilimali na Maliasili za Zanzibar zipo , zitawanufaisha wazanzibari si vinginevyo " Alisema Mbeto.
Kwa muktadha huo ,CCM kimewataka wananchi wa Zanzibar na wafuasi wa ACT, kuamka na kuyatafajari maneno ya Jussa kila anapotamka kwani ameamua kuwa komedi wa kisiasa akiamini atawachekesha walionuna.
'Serikali ya awamu ya nane imejenga Viwanja vya soka vya kisasa , imeimarisha studio za Sanaa na Wasanii. Zimejengwa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Amali ,Zahanati , hospitali za wilaya na Mikoa " Alisema Mbeto.
Mbeto alimtaka Jussa kama kweli yeye si kibaraka ,ajitokeze akanushe kama ACT haikuahidi ahadi hizo.
Alisema CCM kupitia ilani yake ya uchaguzi mwaka 2020 hadi 2025 chini ya serikali ya Rais Dk Mwinyi imetimiza wajibu wake .
"Wana ACT wasidanganywe na Ian Smith . Waisome ilani yao ya uchaguzi mwaka 2020 -2030 waone kama yaliotekelezwa na SMZ kama si yale yaliomo kwenye ilani yao . Jussa si kibaraka tu ni kiongozi mawenge ' Alisisitiza Mbeto
Hakuna maoni
Chapisha Maoni