TAKUKURU MKOANI PWANI YAKAGUA MIRADI YA BILIONI 43.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Christopher Myava
Na Mussa Augustine, PWANI
Taasisi ya kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Pwani, imefanikiwa kukagua miradi ya Maendeleo ipatayo 167 yenye thamani ya zaidi ya shilingi, bilioni 43 katika kipindi cha Mwaka wa 2023/2024.
Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 20, 2025 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Pwani Bw.Christopher Myava wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na Waandishi wa habari Ofisini kwake.
Bw.Myava amefafanua kuwa ukaguzi huo ulifanyika kupitia ofisi zake tisa za Takukuru Mkoani humo ambazo ni Mafia,Kisarawe, Bagamoyo, Rufiji Mkuranga, Kibaha Vijijini, Kibaha Mji, Ikwiriri, Chalinze pamoja na Kibiti.
"Bagamoyo tulikagua miradi 18 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9, Kisarawe miradi 13 ya shilingi bilioni 5.3, Mkuranga miradi 24 ya bilioni 12.2, Rufiji miradi 10 ya Bilioni 3.5. amesema
"Nakuongeza kuwa "Pia tumekagua miradi 32 katika Ofisi ya Mafia yenye thamani ya shilingi bilioni 5.3, Ikwiriri miradi 10 ya zaidi ya bilioni 1 na laki 6, Chalinze miradi nane ya bilioni 3 na laki 2, Kibiti miradi 25 ya Bilioni 3.8 na Pwani katika Ofisi mbili yaani Kibaha Mji na Vijijini miradi 26 yenye thamani ya shilingi bilioni 6.1, kwahiyo jumla ya thamani ya miradi yote iliyokaguliwa ni bilioni 43,342,632,386.86.
Amebainisha kuwa pamoja na hayo kuna miradi mingine bado inaendelea Kutekelezwa ikiwemo Bagamoyo miradi 18, Kisarawe miradi minne, Mkuranga miradi 23, Rufiji miradi mitano, Mafia miradi14, Ikwiriri miradi nane, Chalinze miradi minne, Kibiti miradi yote 24, Pwani miradi yote 26.
Amesema lengo la kufanya ukaguzi wa miradi hiyo ni kuhakikisha pesa za Serikali zinatumika kikamilifu na thamani ya mradi iendane na thamani halisi ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi husika.
"Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo wananchi, tukiwa kama Takukuru lengo letu ni kuhakikisha kwamba zile fedha zinatumika kikamilifu amesema".amesema
Hata hivyo amesisitiza kuwa katika kuongeza ufanisi wa shughuli zao,wamekua wakishirikiana vizuri na Wananchi kupitia programu ya "Takukuru Rafiki" jambo linalowezesha kupata taarifa za changamoto zinazojitokeza kwenye jamii na kuzifanyia kazi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni