Zinazobamba

PROF.LIPUMBA AANZA KUPANGA SAFU YAKE YA UONGOZI

Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Prof Ibrahim Lipumba amemteua, Rajab Mbarouk Mohamed kuwa Katibu wa Kamati ya itifaki na Udhibiti ya chama hicho.


Prof Lipumba pia amemteua, Juma Wandwi kuwa Naibu Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibit na wataanza kazi mara moja na watathibitishwa na Baraza kuu la Uongozi la Taifa kikao kijacho na uteuzi wa wakurugenzi wengine utatangazwa kwa kadri uteuzi utavyokamilika.


Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Jan. 13, 2024 na kitengo cha Habari na Mawasiliano Cha chama hicho nakubainisha kuwa mwenyekiti huyo wa CUF Taifa  amefanya uteuzi huo kwa kuzingatia Katiba ya CUF- Chama Cha Wananchi ya mwaka 1992 Toleo la 2019, Ibara za 91(1) na 92(1).

Hakuna maoni