JUMUIYA JUMUISHI YA WATU WENYE ULEMAVU YAMSHUKURU DR.SAMIA.
Na Mussa Augustine.
Mwenyekiti wa Jumuiya Jumuishi ya Watu wenye Ulemavu Tanzania Bi.Debora Mushi amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia msaada wa vifaa saidizi watu wenye Ulemavu ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka na kuwathamini.
Ametoa shukrani hizo leo Desemba 31,2024 jijinibDar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye hafla ya kuwapatia vifaa saidizi ikiwemo Viti mwendo( Wheelchairs) iiliyobeba ujumbe wa "Asente Mama ,Umetufikia" iliyoandaliwa na Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao.
Tunamshuku sana Rais Dkt Samia kwasabau tuliondolewa bima ya afya na hivi karibuni imerejeshwa,tulipata shida kwenye matibabu lakini limeonwa hilo likafanyiwa kazi" amesema
Nakuongeza kuwa ,Watu wenye Ulemavu Tanzania wapo milioni 11.9 ambao wamegawanyika katika vyama 13 ,hivyo tunamshukuru kwa kuwa mlezi toka aingie madarakani,tunamuahidi kura milioni nne kutoka Jumuiya Jumuishi kwa watu wenye Ulemavu.
Aidha amesema kwamba wapo kwenye hafla hiyo kwa ajili ya kumshukuru Dkt Samia kwa kuwafikia na kuwapatia vifaa saidizi kwa ajili ya watoto na watu wenye ulemavu kwa ujumla.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni