ACT WAZALENDO KIMECHUKIZWA WAGOMBEA UPINZANI KUNYIMWA FOMU ZA KUWANIA UONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA
Isihaka Mchinjita
Na Mwandishi Wetu.
Chama cha ACT Wazalendo kimesema wagombea wa vyama vya upinzani katika maeneo mengi nchini wamekuwa wakinyimwa fomu za kuwania uongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 31, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara Isihaka Mchinjita kwenye Mkutano wake na waandishi wa habari uliyofanyika makao Makuu ya chama hicho Jijini Dar es Salaam.
Mchinjita amebainisha kuwa wakati mwingine watendaji wa Vijiji na Mitaa wamechukua hatua ya kuwatisha wagombea wa upinzani ili wasichukue au wasirudishe fomu hizo.
"Maeneo mengi wanachama wa ACT wamejitokeza kuchukua fomu lakini wanapewa nakala Moja na hivyo wanatakiwa wakatoe "photocopy, yaani mambo ya ajabu sana haya"amesema Mchinjita.
Nakuongeza kuwa "wasimamia wa zoezi la kujiandikisha wapiga kura walifikia hatua ya kukimbia ofisi na hawapatikani,pia maeneo mengine wasimamizi hudai kuwa wameshatoa fomu kwa wagombea wa ACT huku wakijua sio kweli.
Vilevile amedai kuwa wagombea wamekuwa wakitishiwa kwamba wasichukue fomu wala kugombea,lakini pia kwa waliogombea wakitakiwa wajitoe.
Pia ameeleza kuwa wagombea wamekuwa wakidaiwa vitamburisho vya uraia huku wakitambua kua sio wote wenye vitamburisho hivyo.
Chama hicho kimeitaka Serikali kwa muda uliobaki kuhakikisha wagombea wote kwenye maeneo ambayo zimetokea dosari hizo wanapatiwa fomu na kurejesha bila vikwazo vya aina yoyote.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni