Zinazobamba

SERIKALI KUTOA MIKOPO YA BILIONI TATU KWA WASANII MWAKA HUU WA FEDHA 2024/2025


Na Mussa Augustine
Serikali imesema kuwa  kwa Mwaka huu wa fedha imetenga kiasi cha Shlingi bilioni 3, kwa ajiri ya kutoa Mikopo kwa Wasanii wa kazi za uigizaji Nchini kwa lengo la  kujiendeleza kwenye shughuli zao za Sanaa.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 7, 2024 na Mshauri wa Rais, Angela Kahiruki katika shughuli ya kuwaombea  dua Wasanii ambao wametangulia mbele ya haki, ambayo imepewa kaulimbiu inayosema 'Faraja ya Tasnia Tutawakumbuka Daima'.


"Kikubwa ambacho naweza kusema kwa wasanii kutumia vizuri mikopo inayotolewa na Serikali kwaajili ya kuendeleza vipaji vyenu na kuinua tasnia filamu nchini ili kuleta tija stahiki.

 

Aidha Kairuki  amesema amewataka wasanii kuhakikisha wanarejesha Mikopo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kupata mikopo kama ambavyo imekuwa katika msimu uliopita.


Awali Mwenyekiti Mwenyekiti wa Tamasha hilo Stive Nyerere ameoomba Serikali kuwaunga Mkono Wasanii ili waweze kufikia Malengo yao ya Sanaa.


Amesema kwamba Tamasha la Kuwakumbuka Wasanii walaiotangulia mbele za haki litakua kubwa zaidi kwa siku zijazo kwani linalenga kukumbuka mchango wa Wasanii waliofariki nakuacha pengo kubwa katika Tasnia hiyo.


Hakuna maoni