Zinazobamba

TALGWU YAISHUKURU SERIKALI KULIPA MISHAHARA KUPITIA HAZINA.


      Katibu Mkuu TALGWU Rashid Mtima

Na Mussa Augustine.

Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimeishukuru na Kuipongeza Serikali kwa kuridhia ombi la muda mrefu la Chama hicho la kuwalipa Wanachama wake kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali (HAZINA).

Shukurani na pongezi hizo zimetolewa leo Agost 14,2024 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa TALGWU Bw. Rashidi Mtima wakati akizungumza na        Waandishi wa habari, nakubainisha kuwa wanachama 465 kati ya 645 wameanza kulipwa kupitia HAZINA, kuanzia Mwezi Julai 2024 ambapo hapo awali walikua wakilipwa kupitia mapato ya Ndani ya  Halmashauri.

Mtima ameendelea kusema kuwa hatua hiyo iliyochukuliwa na Serikali itasaidia kuondoa kero za muda mrefu,itaongeza Ari na Morali ya kufanya kazi kutokana na kuondokana na Changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo kutolipwa mishahara kwa wakati,kukosa huduma za Matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutokana na makato kutowasilishwa kwa wakati.

Changamoto zingine ni kutokukopesheka katika baadhi ya taasisi za Fedha,kupata usumbufu mkubwa kipindi watumishi wanapo staafu kutokana na makato ya michango yao kutokuwasilishwa kwa wakati katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii( NSSF).

"Pamoja na pongezi hizi tunaiomba tena  Serikali kuangalia upya na kufanya mchakato ili wanachama wetu 180 waliosalia katika Majiji na Manispaa ambao bado wanalipwa kwa mapato ya Ndani ya Halmashauri  nao waanze kulipwa kupitia Hazina " amesema 

Nakuongeza kuwa" TALGWU tunaomba Serikali kwa kipindi hiki ambacho tunawasilisha ombi la watumishi walio salia nao walipwe na HAZINA,Serikali iwasimamie Wakurugenzi wa Halmashauri kulipa mishahara kwa wakati kama ambavyo inafanya HAZINA.

Aidha amezitaja Halmashauri ambazo bado zinalipa kwa kupitia mapato ya Ndani ni Geita Mji,Ilala Jiji,Manispaa ya Kinondoni,Mbeya Jiji,Jiji la Mwanza,Manispaa ya Temeke,Dodoma Jiji,na Manispaa ya Morogoro ,nakusisitiza kuwa endapo zitalipa mishahara ya Watumishi hao kwa wakati itaondoa ombwe kubwa lililopo katika upatikanaji wa haki stahiki za wanachama 180 waliosalia.

Hakuna maoni