Zinazobamba

SERIKALI INAHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HAKI ZA FIDIA KWENYE MIRADI-KAMISHNA SHULI.

Na Mussa Augustine.

Serikali ya Tanzania inafanya  jitihada za kuhakikisha Wananchi wake wanapatiwa haki raslimali katika maeneo ambayo yanapotokea na Miradi ikiwemo ya wawekezaji au serikali ili kusaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa Wananchi.

Matamshi hayo yametolewa Agost 29,2024 Jijini Dar es salaam na Kamishana wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nyanda Shuli, katika Mdahalo ulioandaliwa na taasisi ya Haki raslimali ambapo amesema tume hiyo imekuwa ikifanya kazi na wadau mbalimbali ikiwemo kituo cha Sheria na haki za Binadamu(LHRC) na imekuwa ikipokea malalamiko ya aina tofauti tofauti kutoka kwa Wananchi nakuyaripoti Mahakamani kupatiwa utatuzi.

Katika Mdahalo huo wa walijadili kwa kina namna sheria zinavyoweza  kumsadia mwananchi kupata  haki zake pale mradi unapopita katika eneo lake aliowe fidia kulingana na hali halisi ya  mali zilizopo

"Kuna baadhi ya mikanganyiko inayotokea wengine kutoridhika na fidia wanazolipwa hivyo kuamua kupeleka malalamiko mahakamani,hivyo inatakiwa elimu iendelee kutolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali"amesema Shuli

Kwa upande wake Mwakilishi  kutoka Mradi wa  Bomba la Mafuta Gafi kutoka Unganda hadi Tanzania(ECOP) Fatma Msumi amebainisha kuwa  baadhi ya maeneo ambayo bomba hilo limepita Wananchi wamepatiwa stahiki zao kwa mujibu wa sheria za haki za Binadamu.

"Vingine ilitulazimu kukutana na wazee wa kimila kwanza kuzungumza nao kutokana na baadhi yao imanani zao na matambiko yao hufanyika kwenye makaburi au miti hivyo wengine kukataa kabisa kuhamisha makaburi yao na kuwalazimu wao kuangalia namna ya kukwepa maeneo hayo ili kusitokee mkanganyiko' amesema

Nakuongeza kuwa "Kiukweli  Mradi huu wa bomba la mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kila maeneo ramani yake imeonyesha litapita kuna ofisi ambayo watumishi wake wamekuwa wakizungumza na viongozi wa kijiji, kitongoji ,kimila kuweka mazungumzo ya pamoja kuhusu raslimali zao kama kuna uwezekano wa kulipwa fidia wapishe maradi "

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka  kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)Joyce Komanya amesema kituo hiko kimekuwa kikipokea malalamiko mengi ya ukiukwaji wa haki rasilimali kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa na wawekezaji kutoka Ndani na Nje ya Tanzania kutokana na baadhi yao kulipa Wananchi  fidia ndogo ikilinganishwa na thamani ya mali walizonazo
Hata hivyo baadhi ya Wadau walioshiriki Mdahalo huo akiwemo Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wauzaji wa Madini Tanzania( TAMIDA)ambaye pia ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya  Uuzaji wa Madini ya  GEM Tanzanite Bw. Osman Abdulsattar Tharia ,amesema kuwa kumekuwepo na tatizo la baadhi ya wawekezaji wa nje kutumia Vibali vya wawekezaji wa Ndani na inapotokea wanafanya makosa , wawekezaji hao hukimbia na kuwachia matatizo wazawa Wanaofanya nao kazi.

"Naomba BRELA waangalie hili manake limekua changamoto kubwa kwa wachimbaji wa Madini wa Ndani,manake wanakua wamechukua Lesenj kwa namba zao za NIDA na inapotokea tatizo kwenye Mradi  hawa wawekezaji wa kigeni wanakimbia na kuwachia matatizo" amesema Osman


Hakuna maoni