Zinazobamba

RWEIKIZA AIPONGEZA SERIKALI YA DR.SAMIA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MRADI WA SGR

                               Jasoni Rweikiza

Na Mussa Augustine.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndongo imet metembelea shirika la Reli Tanzania( TRC) kwa ajili ya kujadiili kanuni za watoa huduma  binafsi kutumia Miundombinu ya Reli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agost 3,2024 jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea Shirika hilo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jason Rweikiza amesema kwamba ushirikishwaji wa sekta Binafsi utaleta tija kwa TRC na Kuinua Uchumi wa Taifa.

Aidha Mwenyekiti huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Mradi wa SGR kwani umeleta chachu ya kurahisisha usafiri.

"Tumeelezwa kuwa treni hii kwa safari moja inasafirisha abiria masaa matatu na dakika kidogo wanakuwa wamewadili dodoma na kuendelea mashughuli zao za kijamii na kiuchumi,usafiri huu una bei nafuu" amesema Rweikiza


               Naibu Waziri Uchukizi David Kihenzile

Kwa Upande Wake Naibu Waziri Uchukizi David Kihenzile amesema kwamba serikali imeamua kushirikisha sekta Binafsi  kwenye mradi huo kutokana na serikali kutekeleza miradi mingi ya gharama kubwa.

"Serikali ina miradi mingi inayotekeleza ya gharama kubwa,hivyo kushirikisha sekta Binafsi itawezaesha kupunguza mzigo serikalini na kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati,mfano mzuri Reli ya TAZARA ambayo imeshirikishwa sekta binafsi ambayo inapitisha mizigo yake kwa zaidi y asilimia sabini" amesema Kihenzile 

Aidha ameongeza kuwa maelekezo  yaliyotolewa na Kamati hiyo ,iliyojielekeza kuangalia masuala ya ulinzo na usalama katika reli hiyo wameyapokea nakuahidi kuyafanyia kazi ipasavyo.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa TRC Lameck Magandi amesema kwamba TRC ndiyo mara yake ya kwanza kuingia kwenye uendeshaji wa Reli kwa kushirikisha sekta Binafsi, ili na wao washiriki katika uendeshaji wa Reli hiyo.

Hata hivyo Magandi amesema kuwa tayari Wadau mbalimbali wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya reli, hivyo kinachosubiriwa ni ukamilishaji wa baadhi ya sheria ili mradi huo utakapokamilika sheria hizo ziwe tayari kuanza kutumika
 


Hakuna maoni