Zinazobamba

ABIRIA WALIOFANYA UDANGANYIFU WA TIKETI SGR WACHUKULIWA HATUA

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano Shirika la Reli Tanzania (TRC) Jamila Mbarouk akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Na Mussa Augustine.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limeshawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka Mahakamani na kuwapiga faini abiria wa Treni ya Umeme (SGR) waliobainika kuhujumu Shirika hilo kwa kukata tiketi zinazoonesha wanashukia vituo vya njiani, badala yake wanapitiliza hadi mwisho wa Treni kwa safari za Dar es Salaam hadi Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari  leo Agosti 16, 2024 Jijini Dar es Salaam  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano TRC Jamila Mbarouk amebainisha kuwa siku chache baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro kueleza juu ya hujuma hiyo ambapo baadhi ya abiria wamekuwa wakikata Tiketi za hadi Thamani ya shilingi 1000 ambazo zinawafanya washuke vituo vya njiani lakini wamekuwa wakifika hadi mwisho wa Safari.

Jamila amesema Kutokana na Changamoto hiyo Shirika limechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa tiketi Wakati wa kupanda Treni, Wakati wa Safari na hata Wakati abiria anaposhuka kituo cha mwisho wa safari yake.

"Eneo utakalopandia treni utascan tiketi yako,ndani ya treni pia wakaguzi wanafanya ukaguzi wa tiketi pia wakati wa kushuka unatakiwa kuscani ili kubaini kama kuna udanganyifu wowote, kama itakuwa kuna abiria kafanya udanganyifu basi alamu zitapiga kelele hivyo walinzi watakuja kuangalia kuna shida gani," amesema.

Nakuongeza kuwa"Vituo ambavyo vimebainika kuwa na changamoto hiyo kwa kiwango kikubwa ni Ngelengele na Ruvu ambapo Shirika kwa kushirikiana na vyombo vya usalama tulifanya uchunguzi na kuwabaina abiria hao na kuwachukukulia hatua.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Kitengo Cha Mawasiliano na Uhusiano TRC amebainisha kuwa wamewakamata watu kadhaa waliokuwa wanakata tiketi nyingi kwa wakati mmoja na kwenda kufanya udanganyifu huo.

Aidha ameongeza kuwa Kwasasa ili kupanda treni ya SGR ni lazima uwe na kitambulisho chochote kinachoonesha sura ya muhusika na jina lake kamili.

Aidha amewataka abiria kuwa waadilifu kwa kulinda mali ya umma na kuhakikisha kila mtu anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kuwafichua wanaohujumu na kusisitiza kuwa kwa yoyote atakayebainika kuhujumu shirika atachkuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwemo kufikishwa Mahakamani.

Hakuna maoni