VIJANA REAL ESTATE YAZINDUA MRADI WA VIWANJA KIBAHA SOGA,WANANCHI WAOMBWA KUCHANGAMKIA FURSA
Na Mussa Augustine.
Kampuni inayojihusisha na Uuzaji wa Viwanja ya Vijana Real Estate imezindua Mradi mpya wa Viwanja Kibaha SOGA ikiwa ni kuwasaidia watanazania kupata viwanja kwa bei nafuu.
Aidha ameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha ujenzi wa Mradi wa treni ya Mwendokasi (SGR) kwani unarahisisha Usafiri wa kufika kwenye eneo la Mradi huo
"Tuna viwanja vyenye ukubwa wa upana na urefu wa mita mia nne na mia nane,ambapo vinauzwa kwa mkopo wa shilingi milioni moja na laki nane kwa Mwaka,lakini pia watakaolipa taslimu watapewa punguzo ya shilingi laki tatu hivyo watalipa milioni moja na laki Tano"amesema
Nakuongeza kwamba Waandishi wa habari watapewa ofa ya milioni moja na laki sita kwa Mwaka kwa kulipa kidogo kidogo hivyo amewasihi kuchangamkia fursa hiyo.
Kwa Upande Wake Balozi wa Mradi huo Salim Kikeke ambaye ni mtangazaji mstaafu wa BBC Swahili amesema kwamba ameamua kurudi Tanzania ili kufanya kazi pamoja na Watanazania ya kujenga Taifa.
Amesema kuwa ujenzi wa nyumba na uuzaji wa viwnja ni ishara kuwa uchumi wa nchi umekua hivyo amewasihi watanazania kuchangamkia fursa ya viwanja kutoka Vijana Real Estate.
"Kutoka Dar es salaam hadi Soga ni dakika arobaini tu kwa treni ya SGR,hivyo kutoka kituoni hadi kwenye eneo la Mradi ni kilometa mbili ambapo sio mbali na eneo la makazi" amesisitiza Kikeke.
Aidha ameongeza kwamba mteja anaponunua kiwanja au eneo anapatiwa hati miliki bure kutoka Kampuni ya Vijana Real Estate na anafanya malipo kidogo kidogo au kwa mkupu(full payment)
Hata hivyo Kampuni hiyo ya Vijana Real Estate imetoa viwanja viwili kwa washindi wanaofuatilia zaidi kwenye mitandao yao ya kijamii na kupata comment nyingi kufuatia ujumbe usemao" tukutane Soga" uliochapishwa na Kampuni hiyo.


No comments
Post a Comment