Zinazobamba

AZANIA GROUP YAIPONGEZA SERIKALI


Na Mussa Augustine.

Kampuni ya Azania Group Ltd. imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili waweze kutekeleza majukumu yao bila vikwazo vyovyote.

Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 26,2024 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Biashara Kutoka Azania Group Bw.Joel Laiser wakati wa Uzinduzi wa bidhaa mpya ya tambi ya rangi ya dhahabu( Spaghetti) inayozalishwa na Kampuni hiyo.

"Nitoe shukrani kwa serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa  usikivu mkubwa katika kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji hapa Nchini" amesema Mkurugenzi huyo.

Nakuongeza kuwa,"Serikali imeboresha miundombinu ya bandari pamoja na barabara kwa ajili ya kusafirisha bidhaa mbalimbali pamoja na kuweka vizuri miundombinu ya Umeme na Maji ambayo ni muhimu kwa uwekezaji wa Viwanda.

Amesema kwamba Azania Group imekua wachangiaji wakubwa wa Kodi kwa serikali,pamoja na kutengeneza ajira nyingi,na kufanya uzalishaji mkubwa wa   bidhaa ambazo zinakuza uchumi wa Taifa la Tanzania.

Amefafanua kuwa bidhaa hiyo ya tambi aina ya Spaghetti ina sifa nyingi ikiwemo rangi ya dhahabu( Organi Wheate),nakwamba  haishikamani kama tambi zingine, pia unaweza kula bila kuweka chochote kama kifungua kinywa au Chakula Cha mchana.

Nae Hamisa Mobeto ambaye amepewa Ubalozi wa kutangaza bidhaa hiyo amesema kuwa bidhaa za Spaghetti zinazozaloshwa na Azania Group ni nzuri kwani hazibadiliki rangi yake ya dhahabu na zina radha ya kuvutia.

" Naomba mniamini nitafanya kazi kubwa ya kuwafikishia taarifa hizi wapenzi wa Chakula aina ya tambi,kwa kweli hata mimi nimeitumia tangu iingie sokoni kwa miezi sita Sasa" amesema Mobeto.

Hakuna maoni