Sanlam investment kushirikiana na Benki ya CRDB Kuja na Sanlam pesa Money Market Fund
Kampuni ya Usimamizi wa mitaji Sanlam investment inayofanya kazi katika Nchi 25 za Afrika Mashariki imeanza rasmi kufanya kazi nchini Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya CRDB ikilenga kutoa fursa kwa Taasisi,Vikindi na mtu mmoja mmoja kuwekeza kupitia mfuko maalum wa Sanlam pesa Money Market Fund unaotoa faida ya gawio kulingana na mtaji.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Sanlam investment jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wa Masoko na Usalama wa Mitaji Nicodemus Mkama ametoa wito kwa watanzania kutumia Fursa ya kuwekeza kupitia mfuko Sanlam Pesa money utakao wawezesha kukuza mitaji na kupata mikopo itakayo wawezesha kupiga hatua za Maendeleo
Ameongeza kuwa Sanlam inatoa fursa kwa watu wenye mitaji midogo kukuza mitaji yao kwa kuwekeza kuanzisha shilingi elfu 10 ambapo gawio watakalo pata litapelekea mitaji kukua na kujikuta wakitimiza Malengo waliyo jiwekea na kukuza uchumi wa Familia.


No comments
Post a Comment