Zinazobamba

JEMEDARI SAID KAZUMARI ATEULIWA KUWA CEO WA TIMU ZA JKT TANZANIA


 Na Mwandishi Wetu

Mchambuzi nguli wa Michezo hapa nchini Jemedar Said Bin Kazumari ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu za Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), hapa nchini ambapo ataongoza timu za Jeshi hilo ambazo ni JKT Tanzania na JKT Queens.

Taarifa hiyo imetolewa leo  Jijini Dar Es Salaam  na Afisa Habari wa Klabu hizo Masau Bwire wakati akizungumza na Waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi hilo nakusema kuwa Jemedari Said ameteuliwa kuwa mtendaji mkuu wa vilabu hivyo kuanzia Sasa ili kuendelea kuvipeleka katika mafanikio ya soka hapa nchini.

Aidha katika hatua nyingine Klabu ya JKT Tanzania imemtangaza aliyekuwa nahodha wa Timu ya SIMBA John Bocco kama mchezaji wa Klabu hiyo kwa Msimu ujao utakaoanza rasmi Mwezi Agost.

Aidha Masau Bwire ametangaza mabadiliko ya uongozi ndani ya Klabu hiyo ambapo Mlezi wa timu zote Mbili atakuwa ni Brigedia Jenerali Hassan Rashid Mabena huku Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini akiwa ni Kanali Gofray Mvula 

No comments