
Na Mussa Augustine
CHAMA cha NCCR Mageuzi
kinamtuhumu aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia aliposimamishwa
uongozi na mkutano mkuu ulifanyika Septemba 24 mwaka 2022 jijini Dodoma kwa
utovu wa nidhamu na uporaji wa Mali za chama.
Taarifa hiyo imetolewa
leo Julai 8,2024 jijini Dar es salaam na
Kaimu katibu Mkuu wa chama hicho Faustian Sungura ambapo pamoja na mambo
mengine amesema kuwa Mkutano Mkuu
uliuagiza uongozi wa chama kumchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha Mali alizopora zinarejeshwa kwenye chama.
"Baada ya chama
kukusanya vielelezo na ushahidi kilianza kumchukulia hatua James Mbatia kwa kwenda
wilaya ya kipolisi machi 28 hadi 29 mwaka huu kwa ajili ya kufungua jalada la
kujimilikisha nyumba mbili za chama na kujipatia sh 67000,000 kwa njia za
udanganyifu,"amesema Sungura
Nakuongeza kuwa” Chama
hakikubaliani na hujuma hizo na tumefanya utaratibu kushirikisha jeshi la polisi kuweza kufuata
Mkondo wa Sheria,pia tumetumia njia nyingine
ya kurejesha nyumba 2 ambazo ni mali ya chama.
Hata hivyo chama cha
NCCR Mageuzi kimewataka wapangaji wote waliopo kwenye nyumba hizo waondoke kabla ya julai 30 mwaka huu ili kupisha
ukarabati mkubwa unaotarajiwa kuanza kufanyika agosti Mosi mwaka huu.
Aidha Sungura amesema kuwa ofisi ya RCO wa kinondoni kumlinda James
Mbatia ili asifikishwe mahakamani chama bado kina imani na ofisi ya mwendesha
mashtaka ( DPP )wa mkoa wa Kinondoni kuhakikisha Mbatia anachukuliwa hatua za
kisheria.
“Tunakwenda kufungua
jalada dhidi ya James Mbatia, kwa kupora na kuuza shamba la chama lenye ukubwa
wa hekari 56 katika Kijiji cha kiromo wilayani Bagamoyo.ambapo CAG
amethibitisha kuwa halikuwa na Mali ya James Mbatia.
No comments
Post a Comment