
Jaji Francis Mutungi
Na Mussa Augustine.
Vyama Vya Siasa Nchini Vimetakiwa
kuepukana na Migogoro ya Kisiasa kwani inapasua vyama na taifa kwa
ujumla.
Matamshi hayo yametoklewa
leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini Jaji Francis
Mutungi wakati akifungua mafunzo ya siku
mbili kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini ikiwa yenye lengo la kujenga mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji
wa vyama hivyo.
Jaji Mutungi amesema
vyama vya siasa ni Taasisi ya Umma hivyo vinapaswa kusajiliwa na kutenda Majukumu
yanayotambulika kidemokrasia na kuachana na vurugu ambazo zinasababisha vyama
hivyo kuwa na mpasuko.
"Haya Mafunzo
yatasaidia kuepukana na mambo mbalimbali ikiwemo Mogogoro ya ubadhilifu wa fedha
za chama nakusababisha kuingia kwenye
matumizi mabaya ya fedha za chama hali ambayo imekua ikiripotiwa mara kwa mara
kwenye taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)amesema
Jaji Mutungi.
Aidha, amevitaka vyama
vya siasa kuwa vinara wa kujenga nchi na kwamba Tanzania sio nchi ambayo
inapata utawala kwa mabavu bali ni demokrasia iliotukuka.
“Mkifanya mema wafuasi
wengi watawafuata,mkifanya maovu hakubna atakaewafuata,naomba sana nitoe wito
kwenu muawambie wafuasi wenu waepukanae na migogoro na badala yake walinde
amani ya Taifa”amesisitiza Jaji Mutungi
Ado Shaibu
Kwa upande wake,
Katibu Mkuu wa Chama Cha ACT - Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa migogoro ya
vyama vya siasa inapaswa kutatuliwa kwa njia ya maridhiano na sio kutumia nguvu
zisizofaa.
"Ni kweli Migogoro
inapasua vyama ,hivyo ni vyema vyama kutatua mihogoro kwa njia ya maridhiano,
tunaishukuru ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kutuletea mafunzo haya ili
kuondokana na Migogoro kwenye vyama vyetu vya siasa "amesema Katibu Mkuu
huyo wa Act Wazalendo.
Philipo Fumbo
Naye, Mwenyekiti Taifa
wa Chama cha Demokratic Part (DP) Philipo Fumbo ameishukuru ofisi ya Msajili wa
Vyama Vya Siasa kwa kuandaa mafunzo hayo
,huku akibainisha kuwa vyama vingi vya upinzani havina ruzuku kutoka serikalini
hali ambayo inachangia kushindwa kuajiri
wahasibu na maafisa ununuzi nakupeleeklea migogoro ndani ya vyama kutokana na matumizi
mabaya ya fedha.
Mafunzo ya Siku Mbili
Kwa Viongoz wa Vyama vya Siasa yamelenga katika maeneo mbalimbali imkiwemo
kujifunza kuandaa Taarifaya fedha ya kuawasilisha kwa CAG,pamoja na kuandaa Matamko
ya Mali za Chama hadi kufikia Mwezi
Septema Mwaka huu.
No comments
Post a Comment