Zinazobamba

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA KUFANYIKA MEI 18,2024,WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA


Na Mussa Augustine.

Dar es salaam.

Maadhimisho ya siku ya Afrika ambayo kwa Tanzania yataanza May 18/2024 kwa kufanya Matukio Mbalimbali ikiwemo  mbio za Marathon(AFRICA DAY MARATHON) ili kujumuika na kudumisha umoja wa Afrika.

Hayo yamesemwa May 15,2024 na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Balozi Ally Bujiku wakati wa Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam nakubainisha kuwa wanatambua kuwa michezo ni afya,michezo huleta watu pamoja na michezo hufanya watu wakishirikiana na kuwa na furaha na hiyo itakuwa ni maalumu kwani ni kuazimisha wiki ya Afrika.

Balozi Bujiku ameongeza kuwa  kutakuwa pia na siku maalumu ya Dinner Galar ambapo kila Taifa litawasilisha chakula chake cha asili hivyo kutoa fursa kwa Waafrika wote kuchangamana na kubadilishana uzoefu wa kitamaduni. 

Amesema kuwa katika mtirirko wa matukio hayo pia kutakuwa na Changizo kwaajili ya shule nne za wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Jiji la Dar es salaam lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya elimu ambayo ndio msingi wa Maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi wote Tanzania Ahamada El Badaoui. Mohamed, (Dean of the Diplomatic Corps of Tanzania) ni farahari kubwa kuona Afrika ikiwa pamoja na kuazimisha siku yetu ambapo inatumika kuwa kumbusha kuangazia maswala mbalimbali kama vile kujitahimini juu ya Elimu,afya,viwango vya maisha.

Ameongeza kuwa Kupitia Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan hususani katika kusimamia sekta ya elimu katika kuhakikisha sera ya elimu kwa wote inatekelezeka inatoa mwanagaza kwa waafrika wote kuwa elimu ndio kipaumbele na kitu cha msingi Cha kusimamia

Nao Baadhi ya Mabalozi waliohudhulia mkutano huo akiwemo Balozi wa Morocco in Tanzania ambaye ni katibu wa mabalozi Amesema kupitia Marathon anaahidi kukinbia mbio za urefu wa Km 15 "tunakimbia huku tukiimba kwa pamoja kuwa wamoja zaidi na kuzielekeza dhamira zetu katika kutatua changamoto zetu".

Nae Balozi wa Kenya Nchini Isaac kenda amesema mabalozi kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje wameweka marathon ili kuwaunganisha watu wengi zaidi na ameahidi kushiriki kwenye marathoni hiyo.

" Itakuwa ni dhambi kubwa mimi kutoshiriki kwenye marathoni hiyo kwani kenya inatambulika kimataifa jinsi inavyofanya vizuri,sikuwa nimefanya maamuzi nikimbie umbali gani lakini Balozi mindi amenichochea nitakimbia Km 15 " 

Aidha amewataka watu wengine wengi zaidi wajitojeze katika maadhimisho jwa kushirikiana Marathon na changizo kwaajili ya watoto wenye mahitaji maalumu.

Akizungumzia kuhusua ushiriki katika Marathon Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga Amesema washiriki wote wa mbio za Marathon watachangia Tsh 30,000/= kwaajili ya kupata vifaa vya ushiriki. Na mbio zitakuwa za Kilometers 5 na Kilometers 15.

“Maadhimisho hayo kilele chake kilipaswa kusherehekewa May 25 lakini Tanzania kutokana na kuwa Mwenyeji wa mkutano wa Kimataifa wa Baraza Amani na usalama siku hiyo hiyo ikaona isherehekee kabla”amesema Balozi Kasiga.



No comments