Walimu Morogoro Vijini mjitafakari, matokeo kidato cha nne 2023 ni simanzi
Ukweli mchungu ni
kwamba walimu katika shule 29 za halimashauri ya Morogoro wamefelisha Watoto.
Takwimu huru
ilizofanywa na mtandao huu zinaonyesha katika Watoto 2,233 waliobahatika
kufanya mtihani wa kidato cha nne, ni Watoto 18 pekee wamebahatika kupata
daraja la kwanza, wengine 122 wamepata daraja II, 183 Daraja III.
Idadi kubwa ya watanzania
wenzetu hawa wamejikuta wakiishia daraja la IV na 0. Unaweza ukalia lakini ndio
ukweli huo. Bado haijaeleweka wazi tatizo ni nini lakini ni wazi kuwa anayekutwa
na Ngozi ndio mwizi mwenyewe.
Ukiangalia matokeo hayo
wanafunzi 1,253 wamepata daraja la IV, na waliopata daraja 0 ni 657. Kwa tafsiri
rahisi ni kwamba Watoto 657 walikwenda kuku ana 1253 hawajui hatma yao.
Masikini vijana hawa,
Watoto wa wakulima ambao walipoteza mrasilimali zao vijana wao wakatusue,
walimu na mifumo imewaangusha, nani wa kuwafuta machozi.
Viongozi ambao
tumewachagua, mnafanya nini kufuta vilio hivi huko Morogoro, inaumiza sana
kuona watu wanapigania elimu yenye ubora lakini bado Wilaya hii imekuwa na
matokeo ya kushangaza
Ndugu yangu Taletale,
unajivunia nini kwa matokeo haya, angalia Mwenzako wa Manonga, Bw. Seif
Gulamali. Katika Jimbo lake ameweza kutokomeza 0 kwa asilimia 90. Unazani mtu
kama huyu akirudishwa tena mjengoni kuna atakayepiga kelele, vipi wewe bosi. Hii
nifedheha kubwa unayostahili kujitafakari.
JImboni Manonga, tokomeza
Sifuri (Division 0) imefana kwa zaidi ya 90, katika shule 20 waliopata 0 ni
wanafunzi 6 pekee, Daraja la I ya Point 7 ziko 5. Ziba ziko 2, St Thomas iko 1,
St Margaret iko 1, na Umoja iko 1. Shule Zaidi ya 9 Hazina Mwanafunzi Aliepata daraja
0.
Shule hizo ni pamoja
na Ziba, Choma, Mwisi, Simbo, Ndembezi, Ngulumwa Igoweko, Misana na Ibologero.
Kazi hii si Ndogo ni
Kubwa sana Pongezi Ziende kwa Walimu wao, Hakikawamefanya kazi kubwa mpaka leo
nimeamua kuwafanya kioo ukilinganisha na matokeo yetu, yaani walimu hawa hawana
baya, natamani niwahamishe kule waliko waende Morogoro wakatusaidie japo kwa
mwaka mmoja
Mimi siamini kuwa
wanafunzi na wazazi wa wilaya hii hawajui umuhimu wa Watoto wao kusoma, ndio
maana unaona idadi ya Watoto waliofanya mtihani wa mwisho ni wengi, Zaidi ya
wanafunzo 2233, wazazi wamepeleka Watoto shule shida iko sehemu na dawa
inatakiwa kupikwa kwa walati
Idara ya Elimu
Sekondari mko wapi, mipango ya elimu na mikakati yenu kuinua taaluma Wilaya hii
imekaaje, sisi wachumia tumbo tunaumia tunapoona matokeo hay ana hakuna mtu
anayechukuliwa hatua. Watu wanafunika kombe mwanaharamu apite. Lazima awepo mtu
wa kumfunga kengere Paka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni