Zinazobamba

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya ziara ya kitaifa Vatican


 Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara ya kitaifa Vatican kuanzia February 11 – 12, 2024 kufuatia mwaliko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba akiongea leo Dar es salaam amesema dhumuni la ziara hii ni kuimarisha ushirikiano wa uwili kati ya Tanzania na Vatican “Itakumbukwa mwaka 2016 Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, alimwalika Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, yaani Baba Mtakatifu Francis kutembelea Tanzania hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya ziara hiyo haikuwezekana na badala yake kwa wakati huu, Rais Samia amealikwa na Kiongozi huyo kufanya ziara Vatican”

“Akiwa Vatican Rais atakutana kwa mazungumzo na Baba Mtakatifu Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Pietro Parolin lakini kabla ya ziara ya Vatican Rais pia atafanya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia January 24 – 26 kufuatia mwaliko wa Joko Widodo, Rais wa Jamhuri ya Indonesia, ziara hii ya Kitaifa inafuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Joko Widodo aliyoifanya Tanzania mwezi Agosti 2023” Alisema Waziri Makamba.

Rais Samia pia atafanya ziara ya Kitaifa nchini Norway, February 13-14, 2024, kufuatia mwaliko kutoka kwa Mfalme Herald wa Norway na Malkia Sonja ikiwa ni miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Nchi hiyo. 

Hakuna maoni