Zinazobamba

BODI YA SUKARI YAWAONYA WANAOPANDISHA BEI YA SUKARI,YACHUKUA HATUA KUKABILIANA NA UHABA WA SUKARI


 

Mkurugenzi Mkuu  Prof. Kenethy Bengesi

Mussa Augustine

 Serikali kupitia Bodi ya Sukari Tanzania  imewataka wafanyabiashara wanaouza  bei ya sukari isiyo halali kuacha mara moja na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 Onyo hilo limetolewa leo Januari 18,2024 Jijini Dar  es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof. Kenethy Bengesi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa Bodi hiyo imebaini kuwepo kwa  baadhi ya wafanyabiashara ambao siyo waaminifu wanaouza sukari kwa bei isiyo halali nakuwafanya wananchi kushindwa kumudu gharama hiyo.

" Bodi inatambua kuwa kila Mkoa bei ya Sukari inatofautiana hivyo Wafanyabiashara wanaopandisha bei kwa maslahi yao binafsi tofafauti na bei halali iliyopangwa na serikali waache mara moja ,tutawachukulia hatuta kali za kisheria kwani hatupendi kuona wananchi wakilalamika kupanda kwa bei ya sukari “amesema Mkurugenzi huyo

 Akizungungumzia kuhusu uhaba wa sukari uliopo kwa sasa Prof. Bengesi amesema haliyo imetokana na kunyesha mvua za Elinino zilizoanza mwezi Oktoba 2023 na kupelekea mashamba ya miwa kujaa maji pamoja na Miundombinu ya barabara kuharibika hivyo kushindwa kuvuna miwa iliyotakiwa kupelekwa kiwandani kusagwa ili kupata  sukari .

 " Mwaka huu tumezalisha tani  laki tatu na elfu arobaini na tano pekee ambapo hazitoshelezi lakini kawaida mahitaji huwa ni tani laki tano na ishirini,  na katika uzalishaji tumejiwekea  malengo yetu ni kuzalisha tani laki tano na hamsini na tano ili tuwe na akiba ya sukari ya kutosha lakini kutokana Msimu huu wa mvua za Elinino tumeshindwa kufikia lengo ndiyo maaana tuna uhaba wa sukari" amefafanua Bengesi mbele ya Wanahabri

 Hata hivyo amebainisha Serikali imechukua hatua za kukabiliana na uhaba wa sukari kwa kutoa kibali kwa kuagiza sukari nje ya nchi tani elfu hamsini na kwamba sukari hiyo inatarajiwa kuingia nchini kuanzia  januari 22 , mwaka huu.

 

 

 

Hakuna maoni