Zinazobamba

MAKAMBA:SERIKALI INATAMBUA UMUHIMU WA KUSHIRIKISHA WANANCHI KATIKA MASUALA YA KITAIFA.

             Waziri Januari Makamba 

Na Mussa Augustine.

Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Januari Makamba amesema serikali inatambua umuhimu wa wananchi kushiriki katika Maamuzi yanayohusu masuala ya kitaifa na kimataifa ikiwemo utoaji wa maoni kuhusu marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya nje ya mwaka 2001.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo Januari 9,2023 jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la kukusanya maoni ya wadau mbalimbali kuhusu mapendekezo na Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya nje ya mwaka 2001.

Amesema Kwamba kuna umuhimu wa wadau mbalimbali ikiwemo wanasiasa Asasi za kiraia viongozi wa dini kushirikishwa wa kutoa maoni yao mahsusi katika mchakato wa marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.

" Nchi ya Tanzania kama yalivyo Mataifa mengine,ambayo nchi zao zinavyokabiliwa na fursa na changamoto katika ushiriki wake kwenye jukwaa la kimataifa,hivyo ni vema kuwa na sera madhubuti ambayo ni muhimu katika kutumia ipasavyo fursa hizo na kukabiliana na changamoto ambazo zitajitokeza,”amesema Waziri Makamba

”Kuna umuhimu wa kupata maoni mbalimbali yanayotolewa na wadau katika kuwezesha uwepo wa sera yenye tija ,itakayokidhi matarajio ya wananchi.

Aidha amesema kuna umuhimu wa kupata maoni ya sera hiyo ili kuwezesha taifa kunufaika ipasavyo na fursa zitokanazo na ushirikiano wa kikanda na kimataifa hasa utekelezaji wa dhana ya diplomasia ya uchumi kwa maendeleo endelevu na Mustakabali wa Taifa pasipo kuathiri wananchi wake 

Aidha amesema ndani ya kongamano hilo wadau hao watapata fursa ya kuelewa kwa kina masuala muhimu yaliyomo katika sera ya mambo ya nje ikiwemo misingi ya Sera zao na malengo yake.

”Pia wataweza kupata uelewa wa historia ya sera ya mambo ya nje tangu kupatikana kwa uhuru hadi ilipofika mwaka  2001 ambapo utekelezaji wa sera ulianza  mwaka 2001 hadi sasa yanafanyika mapitio ya sera hiyo,”amesema.

Waziri Makamba ameongeza kuwa katika kongamano hilo,wizara yake inapenda kusikia kutoka kwa wadau jinsi wanavyoona marekebisho yaliyofanyika katika sera na ni maoni gani waliokuwa nayo kuhusu njia zitakazochukuliwa kufikia malengo wanayotamani kufikia.

Naye mmoja wa  Viongozi wa Kisiasa waliohudhuria Kongamano hilo Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni mwenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Nchin(TCD) Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwa  sikivu kutokana na kuwashirikisha Wananchi wake katika utoaji wa maoni katika baadhi ya mambo muhimu ikiwemo masuala ya urekebishaji wa sheria.

 

Hakuna maoni