Na Mussa Augustine
Makamu wa Rais Dkt
Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima katika Mkutano Mkuu wa 52 wa jumuiya ya
Waislamu Waahmadiyya Tanzania " JALSA SALANA" utakaofanyika Septemba
29 hadi Oktoba 1 ,2023 Kata ya Msongola Manispaa ya Ilala Mkoani Dar es salaam.
Hayo yamesemwa Mapema leo
Septemba 28 ,2023 jijini Dar es salaam na Naibu AMir ( Deputy Head) Abdulrahman
Mohammed Ame kwa niaba ya Amir and Missionary Inharge Ahmadiyya Muslim
Jamaat Tanzania wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea
Mkutano huo.
Amesema kwamba
kupitia Mkutano huo waumini watapata nafasi ya kusikiliza hotuba na nasaha za
wataalamu wa Jumuyiya ambapo miongoni mwa mambo yatakayozungumzwa ni namna bora
ya kuwalea watoto ikiwemo kujali elimu yao ya dini na sekula yaani kujitahidi
kuwa raia wema kwa kuishi kwa amani na watu wote na kuwa watiifu kwa sheria za
nchi.
Naibu Amir Abdulrahman
ameendelea kusema kuwa katika Mkutano huo waumini watakumbushwa juu ya umuhimu
wa kujiepusha kuchanganya dini na siasa kwani jambo hilo huleta mkanganyiko na
kuzalisha mianya ya ama wanasiasa kuitumia dini vibaya au watu wa dini kuitumia
siasa vibaya kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Aidha amesema kuwa
kauli mbiyu ya Jalsa ya Mwaka huu hapa nchini ni " Tawheed ya kweli
haiwezi kusimamishwa na bila ya Ukhalifa" ikiwa na maana ya kuwa mfumo wa
Ukhalifa ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu tangu zama za Nabii Adam ndio njia
pekee ambayo Mwenyezi Mungu hudhihirisha Umoja wake hapa duniani na leo hii
Tawheed ya kweli itasimamishwa kupitia Ukhalifa ulioanzishwa tena na Mwenyezi
Mungu katika Uislam sawa na ahadi iliyotolewa na Mtume Muhammad s.aw.
Aidha amesema kuwa
Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya ni Jumuiya ya Kimataifa inayopatikana kwenye
zaidi ya nchi 212 duniani ikiwa nchini ya Kiongozi mmoja( Khalifa
Mtukufu)
" Lengo lake kuu
ni kutangaza kwa amani ujumbe sahihi wa Islam duniani kote na kuwa mstari wa
mbele katika kupinga maana zisizo sahihi zinazonasibishwa na mafundisho ya
uislam kama vile dhana potofu za ugaidi na misimamo mikali isiyovumilia wengine"
amesema Naib Amir Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania Abdulrahman
Nakuongeza kuwa katika
mkutano huo viongozi wa kitaifa wa serikali,vyama vya siasa ,viongozi wa dini
mbalimbali na jamii kwa ujumla watashiriki katika kutoa nasaha zao nakwamba
idadi ya washiriki inakadiriwa kuwa 5000 hadi 6000 kutoka maeneo mbalimbali
nchini wanatarajiwa kuhudhuria Jalsa hii ya 52 na pia washiriki kutoka nchi za
Kenya,Uganda na Ghana wanatarajiwa kuhudhuri
Awali akisoma ujumbe
wa Kiongozi Mkuu wa Ahmadiyya Duniani Amir & Missionary
Inharge wa Ahmadiyya Muislim Jamaat Tanzania Tahir Mahmood Chaudhry amesema
kwamba Mkusanyiko huo umejengwa juu ya uungwaji mkono kamili wa ukweli na
uenezaji wa uislam ambapo jiwe la msingi la jumuuiya hiyo limewekwa na mwenyezi
Mungu.
" Nimuhimu kwamba
mnufaike kikamilifu na mwenendo ya Jalsa hii ili kujifunza jinsi ya kuboresha
viwango vyenu vya kiroho na kimaadili , kuwa bora katika kufanya vitendo vya
ucha Mungu ni hivyo kupata ukaribu kwa mwenyezi Mungu Mtukufu " imesema
taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo pia
imeongeza Washiriki wa Jalsa hiyo wanapaswa kuzingatia wajibu wao kuhusu
mahubiri ambayo ni muhimu kwa kila ahmadiyya kupanga nakubuni njia mpya na
zenye hekima kueneza ujumbe wa amani wa Islam ahmadiyya kote Tanzania na nchi
jirani.
Naye Amir Ahmadiyya
Muslim kutoka nchini Ghana Mohammed Bin Salih amesema kwamba amefurahishwa
kupewa mualiko wa kuja kushiriki Jalsa hapa nchini huku akisema kuwa mkusanyiko
huo unasaidia vijana kubadilika kimalezi na kiimani amewasisitiza Watanzania
kujitokeza kushirikia Mkusanyiko huo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni