MANISPAA YA UBUNGO KUFANYA KONGAMANO LA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI KUOKOA MAISHA YA WAHITAJI.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hananja Compasion Foundation, Richard Hananja
Na Mussa Augustine.
Taasisi ya
Hananja Compasion Foundation kwa Kushirikiana na Manispaa ya Ubungo inatarajia Juni 24 Mwaka huu kwa ajili ya Kuhamasisha
Wananchi kuchangia Damu kwa hiari huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa
Wilaya hiyo Hashim Komba.
Akizungumza jijini
Dar es salaam na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Taasisi ya Hananja Compasion
Foundation, Richard Hananja amesema
kwamba Kongamano hil litafanyika katika Senta ya Goba Manispaa ya Ubungo ambapo
amewasihi Wananchi kujitokeza Kwa wingi kuchangia Damu kwa ni Sadaka kwa
Wagonjwa waliopo Hospitalini.
Hananja
ambaye pia ni Mchungaji Mstaafu amesema Kuwa wagonjwa waliopo hospitalini
wanaohitaji Damu ni wengi akitolea mfano wakina mama wajawazito wanaopoteza
maisha wakati wa kujifungua pia madereva wanaopatwa na ajari hivyo ni jambo la
kumpendeza Mungu kuchangia damu kuokoa masiha ya wengine.
“Napenda
kutumia nafasi hii kuwaomba Wananchi wa Goba na maeneo mengine waje siku hiyo
wachangie Damu kwa hiari kwani ni Sadaka,pia tunatoa elimu kwa Jamii kuondokana
na imani potofu kuhusu uchangiaji wa Damu,ambapo Kongamano hili limebeba ujume
wa “Changia Damu Salama ,Okoa maisha ,Goba na Damu salama”amesema Hananja.
Ameongeza
kuwa Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu
Hassani,Makamu wake Dkt Philip Mpango
pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa inatekeleza kaulimbiu yake ya
Kazi iendeleee hivyo vifo vitokanavyo na upungufu wa Damu vinasababisha
kupoteza nguvu ya Taifa nakwamba jamii iwe na utamaduni wa kuchangia Damu kwa
hiari ili kuwa na Damu ya kutosha Mahospitalini.
Mratibu wa Damu Salama Manispaa ya Ubungo Analimi Machalo
Nae Mratibu wa Damu Salama Manispaa ya Ubungo Analimi Machalo amesema kwamba Kongamano hilo nila mara ya kwanza kufanyika katika kata ya Goba lakini wanatarajia kukusanya Uniti 300 za Damu.
“Kumekuwa na uhitaji Mkubwa wa Damu Mahospitalini hivyo Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana nna Wadau Mbalimbali tumekuwa tukihamasiha jamii kua na utamaduni wa kuchangia Damu kwa hiari ili kuokoa Maisha ya Ndugu zao,au watu wengine wenye uhitaji wa damu”amesema Machalo
Pia Mratibu
wa Mradi wa “Afya Yangu” kutoka shirika la Jhpiego USAID Joyce Francis
Ishengoma amesema kwamba shirika hilo limekuwa likishirikiana na Wadau Wengine
kama Taasisi ya Hananja Compasion Foundation kuhakikisha wanatoa huduma za afya
zilizo bora kwa jamii.
“Wakina mama
wajawazito wanapoteza Damu nyingi wakati wa kujifungua,wengine wanapata ajari
na kutokwa damu nyingi hadi kupotezMaisha ,hivyo sisi kama Jhpiego USAID
kupitia mradi wa Afya Yangu tunaotukeleza katika Kanda ya Dar es salaa,Tanga na
Tabora tunashirikiana kuweka mazingira ya huduma bora za afya ili kuimarisha
afya ya Mama na Mtoto” amesema Joyce.
Kikao hicho
kilifanyika katika shule ya Sekondari Goba kawa ajili ya kuweka maandalizi ya
kongamano hilo kimehudhuliwa na Viongozi wa Chama,Walimu pamoja na madereva wa
bodaboda
Hakuna maoni
Chapisha Maoni