Zinazobamba

JAMIIFORUMS YAKUTANA NA WADAU WA HAKI ZA KIDIGITALI KUJADILI CHANGAMOTO YA SHERIA ZA ANGA YA KIDIJITALI.

 Meneja Programu kutoka JamiiForums ,Ziada Seukindo           

Na Mussa Augustine.

Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali Tanzania (Digital Rights Coalition Tanzania)  limeandaa Warsha ya kujenga uelewa kwa Wadau wa Sekta ya Kidijitali kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Anga ya Kidijitali Nchini Tanzania pamoja na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa katika tasnia hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kando ya Warsha  hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Meneja Programu kutoka JamiiForums ,Ziada Seukindo amebainisha kuwa watu wengi wanajipatia kipato kutokana na fursa zinazopatikana Mtandaoni, lakini wanaweza kuathiriwa ikiwa Sheria au ‘Digital Space’ haziendani na  kasi ya ukuaji wa teknolojia kwa ulimwengu wa sasa.

“Mkutano huu ni wa Wadau kujadili changamoto na fursa katika Ulimwengu wa Kidigitali, pia kupendekeza njia za utatuzi wa changamoto hizo ambapo baadae tutaziwasilisha kwa watu ambao tunaamini wanaweza kuzifanyia kazi” Amesema Ziada .

Program Meneja huyo wa Jamiiforums amesema kwamba wanaangazia zaidi Sheria, hasa kwa kuwa wanaamini kwamba ndizo zitakazotoa haki mbalimbali lakini pia zitaweka mazingira rafiki ya watu kutumia vizuri fursa ambazo zipo mtandaoni na kujipatia kipato cha kujikimu katika maisha yao na jamii inayowazunguka.

Amesema kuwa wanafanya uchechemuzi wa Haki za Kidigitali kwa sababu zama za sasa  Watu wengi wanatumia vifaa vya kidigitali na mtandao na Majukwaa ya kidigitali, hivyo utu wa watumiaji upo hatarini.

“Leo hii picha zako, taarifa zako binafsi ziko mtandaoni ambapo Mtu anaweza kuzitumia kwa namna yoyote ambayo inaweza kukuathiri au kuathiri Watu wa karibu yako, kuna haja sheria zetu zikawa vizuri katika kumtetea mhanga tofauti na sasa mhanga nae anakuwa miongoni mwa mtuhumiwa” Amesema Ziada Seukindo

Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya Wadau wa Sekta ya Kidijitali

Nakuongeza kuwa Watu wanajipatia kipato kutokana fursa zinazopatikana mtandaoni, ambapo wanaweza kuathiriwa ikiwa Sheria au ‘Digital Space’ haipo vizuri hivyo sheria zinazosimamaia maadili ya Mtandaoni lazima zisimamiwe vizuri.

Amesema Mkutano huo wa Wadau utajadili changamoto na fursa katika Ulimwengu wa Kidigitali, pia kupendekeza njia za utatuzi wa changamoto hizo ambapo baadaye wataziwasilisha kwa Watu ambao wanaamini wanaweza kuzifanyia kazi.

Ametaja baadhi ya changamoto mbalimbali watakazozijadili kuwa ni Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ikiwemo Tume inayosimamia Ulinzi wa Taarifa Binafsi (The Data Protection Commission) imepewa nguvu kubwa sana ambazo zinaweza kuathiri utendaji kazi wa Taasisi au watu mbalimbali.

“Tume imepewa uwezo wa kuingia kwenye jengo lolote, na kuchukua kifaa chochote ambacho wao wanahisi kina taarifa wanazozihitaji bila kuwa na kibali chochote na pia imepewa nguvu za kutozingatia Sheria zozote wakati wanatimiza majukumu yao, hii ni hatari sana kwa taarifa za watu wengine hususani NIDA ambayo inataarifa za watu wengi kuchukuliwa vifaa vyao kwa ajili ya ukaguzi huku kukiwa na taarifa za watu wengine”Ameongeza Ziada Seukindo.         

Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya Wadau wa Sekta ya Kidijitali

Kwa upande wake Mwakilishi toka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Raymond Kanegene amesema

Digital space ni msingi wa Uhuru wa Kujieleza Duniani ,hivyo ni vyema Sheria zikaakisi katika kutengeneza njia rafiki ya ulimwengu wa Kidigitali.

Amesema teknolojia ya Kidigitali ni msingi wa Uhuru wa Kujieleza. Haki hii ipo kwenye Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kanuni za Maudhui ya Mtandaoni zilianzishwa (2018) na kurekebishwa 2020 na 2022 mtawalia, lengo likiwa kuregulate aina ya maudhui yatakayo kuwa mitandaoni

Ameongeza kuwa Kanuni hizo zikatambulisha prohibited contents, maudhui ambayo hayatakiwi kuwepo mtandaoni. Kanuni hizo zimekuwa zikiathiri ustawi wa Digital Space Tanzania.

Aidha amesema sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2023) inamtaka Mkusanya, Mchakata na Mdhibiti wa Taarifa kusajiliwa na inawataka wakusanya taarifa binafsi wote kusajiliwa kasoro Taasisi za Serikali, ambazo zimesajiliwa automatically.

Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2023) inazuia mtu yoyote kukusanya taarifa binafsi bila kusajiliwa hivyo kama mpenzi wako ataingilia faragha yako kwa kukagua simu yako na ukapata athari unaweza kwenda kwenye tume ya malalamiko (itakayoanzishwa hivi karibuni) kwa ajili ya hatua za kisheria.

Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa (2016) ilitungwa kwa ajili ya kuleta Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa Wananchi
kama Raia unaweza kwenda kwenye ofisi fulani ya Serikali au kutumia mtandao kuuliza kuhusu taarifa fulani.

“Sisi kama Wadau wa Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali, ni jukumu letu kuwezesha matukio yanayotokea ana kwa ana, mfano, Vikao na Warsha mbalimbali kuweza kufanyika kupitia mtandaoni hii ni njia mojawapo ya kuziba pengo lililopo kati ya Ulimwengu halisi na Ulimwengu wa Mtandao” Amesema Bw.Kanegene

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The LaunchPad Tanzania, Carol Ndosi

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The LaunchPad Tanzania, Carol Ndosi amesema kuwa kuendelea kusambaa kwa picha za utupu mtandaoni husababishwa na hali ngumu za kiuchumi hususani kwa wanafunzi wa chuo baada ya kulagaiwa kuwa wakituma picha hizo watapatiwa fedha ndipo baadae husambazwa mitandaoni bila ridhaa yao.

Aidha amesema kwamba kumekua na kesi nyingi zinazoripotiwa katika mamlaka za kisheria lakini hatua hazichukuliwi kwa wahusika wanaoshitakiwa huku sheria pia ikishindwa kumlinda mhanga,hivyo ameshauri kuhakikisha sheria hizo zinasimamiwa ipasavyo.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya Wadau wa Sekta ya Kidijitali



Hakuna maoni