Zinazobamba

Wizara ya Afya Kuendelea kulinda Afya za Watanzania.

 

Na Mussa Augustine.

 Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuhakikisha Afya ya Watanzania inalindwa dhidi ya mlipuko wa magonjwa mbalimbali yanayotokea.

 Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akizidua kituo cha Kanda cha  umahili wa utoaji wa mafunzo ya Ulinzi na Usalama wa vimelea vya magonjwa.

 Aidha Waziri huyo wa Afya amesema kwamba maabara ya Taifa imepewa heshima yakua kituo

cha Kanda cha mafunzo ya ulinzi na usalama wa vimelea  vya magonjwa kutokana kuwepo kwa wataalamu waliobobea katika upimaji wa sampuli mbalimbali za magonjwa.

 " Wizara ya Afya itaendelea kutekeleza mpango mkakati wa  AFRICA CDC wa kuhakikisha  Ulinzi na Usalama wa vimelea kwa kutoa mafunzo ya vitendo kwa wataalam wa maabara ili kuhakikisha kunakuwepo na hatua muhimu za kukabiliana na magonjwa hatari yanayojitokeza ikiwemo Ulinzi,kujiandaa,kujenga uwezo wa kugundua ugonjwa wenyewe kupitia kampuli,pamoja na kuchukua hatua" amesisitiza Waziri Ummy.

 Ameendelea kufafanua Mwezi Septemba 2022 Maabara ya Taifa iliomba kuwa kituo cha Kanda cha mafunzo ya Ulinzi na Usalama wa Vimelea vya magonjwa nakwamba AFRICA CDC imeridhia ombi hilo nakwamba kituo hicho kitatoa huduma kwa nchi zingine za afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda.

"Mpaka sasa tayari vyuo mbalimbali kutoka nje ya nchi vimeomba kuja kujifunza kwa vitendo kwenye kituo hiki,natumaini kupitia kituo hiki wataalamu wa kimataifa wanapata mafunzo kwa gharama nafuu,naomba nitoe wito kwa vyuo vya hapa nyumba kuchangamkia fursa hii ili wajifunze kwa  vitendo" amesisitiza Waziri Ummy.

 Awali Mkurugenzi wa Mipango kutoka kituo cha kudhibiti Magonjwa Afrika (AFRICA CDC) Dkt Talkmore Maruta amesema kwamba kituo cha AFRIC CDC kitaendelea kushirikiana na Kituo Cha Kanda cha Mafunzo ya Ulinzi na Usalama wa vimelea kwa kutoa mafunzo mbalimbali huku aikiipongeza wizara ya Afya ya  Tanzania kwa juhudi kubwa inayochukua kukabiliana  na magonjwa mbalimbali yakuambukiza.

 Katika hatua nyingine Dkt Talkmore Maruta amemkabidhi Waziri Ummy Cheti cha utambulisho rasmi wa kituo cha Kanda cha Mafunzo ya Ulinzi na Usalama wa Vimelea vya magonjwa baada ya kupitishwa na AFRICA CDC kutokana na kukidhi vigezo.

Hakuna maoni