WAMILIKI WA MAGARI YANAYOBEBA WANAFUNZI FANYENI UKARABATI MAGARI YENU MARA KWA MARA
NA Mussa Augustine
Jeshi la polisi Usalama barabarani limewataka wamiliki wa magari yanayobeba wanafunzi kuhakikisha yanafanyiwa ukarabati wa marakwa mara ili kusaidia na ajali zinazosababisha wanafunzi kufariki au kupata ulemavu wa kudumu.
Kamanda wa Usalama Barabarani Nchi Wilbroad Mutafingwa. |
Agizo hilo limetolewa na Kamanda wa Usalama Barabarani Nchi Wilbroad Mutafingwa wakati WA zoezi la Elimu na Ukaguzi wa magari hayo uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Magari yapatayo 100 yaliwasilishwa na wamiliki wa magari hayo Ili kufanyiwa ukaguzi wa mifuno mbalimbali ikiwemo uchakavu wa bodi,Mfumo wa breki, matairi,mpangilio wa viti pamoja na mikanda yakujiunga wanafunzi wakiwa katika safari ya kuenda na kurudi shuleni.
Kamanda Mutafungwa amesema kuwa wameamua kufanya ukaguzi Kwa kipindi hiki ambapo shule zimefungwa ili kuhakikisha ifikapo Septemba 5 siku ya Shule kufunguliwa magari yote ambayo yamekutwa na kasoro yaweze kutengenezwa au kuondolewa Barabarani.
"Wazazi,Wamiliki wa shule,Wasimamizi wa Watoto,wakuu wa shule pamoja na Madereva kushirikiana na Jeshi la Usalama Barabarani katika kuzuia hizi ajari ,hivyo nawataka wamiliki wahakikishe magari ya Shule yanafanyiwa ukaguzi mara mbili Kwa mwaka kama sheria inavyoelekeza" amesema Mutafungwa
Amesema kwamba Madereva ambao hawana leseni daraja C kutoka chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji( NIT) na Chuo Cha Elimu ya Mafunzo ( VETA) hawaruhusiwi kuendesha magari ya Wanafunzi hivyo katika kipindi hiki wanafunzi wakiwa likizo Madereva ambao hawana leseni hizo wanapaswa kujiendeleza kitaaluma ili wapate leseni ya daraja C.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni