Zinazobamba

STAMICO KUADHIMISHA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAWE

Na Musa Augustine

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza kuiadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake huku likitarajia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupanda miti kwenye eneo la ipagala jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)  Dkt Venance Mwasse
Akizungumza na wanahabari  leo Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo  Dkt Venance Mwasse amesema kwamba Maadhimisho hayo yatafikia kilele agost 12 mwaka huu jijini Dodoma ambapo pia zitafanyika shughuli  za kupanda miti na kutoa misaada kwa watu wanaougua saratani ,pamoja nakuwapa vifaa watu wenye ulemavu wakutokusikia.

Dkt Mwasse amesema kwamba  STAMICO ni Shirika ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kujitangaza na pia limepata tuzo katika maonyesho mbalimbali ikiwemo maonyesho ya viwanja vya  sabasaba mwaka jana.

 "Tutapanda miti,na tunafanya maenyesho haya ya kihistoria ya miaka hamsini ,tutafanya matukio mbalimbali yakijamii ili kuhakikisha Mambo yote yapo sawa,na miti elfu kumi tunapanda,amesema Dkt Mwasse
Hata hivyo amesema wamefanya  wa mkaa mbadala ni mradi mkubwa unakwenda kuleta suluhisho la mabadiko ya tabia nchi na utafiti huo ulianza 2018 na ulifanyika katika hatua mbalimbali ambapo 2019 matokeo yalionyesha mkaa huo ungenza kutumikia mtumiaji angetakiwa kutumia sufuria mpya na jiko lisingefaa tena huku sufuria ikiharibika yote hivyo wakaona haifai matokeo hayo yanakwenda kuongeza changamoto ya gharama na isingekuwa rafiki kwa watu wenye kipato cha chini ikalazimu kurudi maabara Hadi bidhaa hiyo ilipofaa

Hakuna maoni