VETA yaeleza thamani ya zao la mbaazi, Watanzania waaswa kulitumia
Mwandishi Wetu
Ukienda viwanja vya sabasaba, jambo la kwanza
utakalolishuhudia ni wingi wa watu, hakika maonyesho ya 46 ya sabasaba kwa mwaka
huu yamekuwa ya aina yake, watu wengi wamejitokeza kwa wingi kujifunza na
kujionea fursa mbalimbali.
Yapo mabanda mengi ambayo ukifika hutamani kuondoka,
miongoni mwa mabanda hayo ni banda la VETA, hakika ni banda ambalo lina mambo
mengi yanayojibu shida za wananchi.
Jana nilifanikiwa kuingia katika banda hilo, nimeona
mambo mengi kuanzia sualala ujuzi, maarifa na ufundi, ni banda ambalo
limesheheni vijana wenye ujuzi wa hali ya juu
Njiro na Zao la Mbaazi…
Ukizungumza zao la mbaazi hapa nchini ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa
kama zao la biashara kutokana na kuwa na soko zuri. Mbaazi ina kiasi kikubwa
cha protini. Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 6 hadi 8 kwa hekta.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mtaalam
kutoka chuo cha Hotel VETA Njiro Happines
James alisema zao hilo ni dhahabu ya kijani ambayo bado haijutumika ipasavyo
hapa nchini.
Kutokana na umuhimu wake kwa jamii, chuo kimeona ni vema
kuwaonyesha watu asili yao, ni chakula ambacho ni muhimu katika kuujenga mwili
na afya ya akili.
“Ttumeleta maajabu ya vitu viwili, navyo ni chakula
ambavyo tunavyo sisi watanzania, zao la kwanza ni mbaazi pamoja na ndizi
kitarasa, kupitia bidhaa hiyo tumeweza kutengeneza biscuiti, keki, mikate, unga
wa mbaazi,” alisema
Tabia ya watu
kuchukulia poa zao la mbaazi
Licha ya kwamba zao la mbaazi ni dhahabu ya kijani, bado
watu wanalichukulia poa zao hilo, kwa muda mrefu sana watu wamekuwa
wakilichukulia poa zao hilo likionekana kama halina faida yeyote, watu wengine
wamekwenda mbali na kulitumia kama alama ya mipaka mashambani.
“Nimekuja huku nimekuta watu wanasema zao hili linatumika
kama dawa ya kufukuzia wachawi mashambani, ni imaani ambazosio sahihi, zao hili
lina faida kemkem katika mwili wa mwanadamu,” alisema
Mbali na kutumika katika imaani za kishirikina lakini pia
watu wengine wamekuwa wakilitumia kama alama ya mipaka ya shamba, ukweli ni
kwamba zao hili lina thamani kubwa, tunaweza sema kuwa zao hili ni dhahabu ya
kijani.
Mtaalamu huyo ambaye amepanga kuandika kitabu kuhusu
umuhimu wa zao la mbaazi, lakini pia umuhimu wa kuthamini vyakula vya nyumbani
alisema angetamani kuona watu wanapata elimu sahihi ya zao la mbaazi na
kulitumia zao hilo kama chakula.
“Tukipenda sana watu wafahamu umuhimu wa zao la mbaazi,
ni moja ya zao ambalo limeonekana kuwa
na faida kubwa sana katika miili yetu, zina imarisha afya ya moyo, zinaongeza
nguvu za kiume lakini pia inarutubisha ardhi,” alisema
Mbali na umuhimu huo pia zao hili linawezesha kujenga
afya ya akili na mwili, tungetamani kuona watoto wetu ambao wanasoma katika
shule mbalimbali waachane na kunywa ujio usio na virutubisho, waachane kabisa
ya uji ambao hauna faida, badala yake wajikite kwenye matumizi ya kunywa uji
uliotengenezwa na mbaazi,” alisema.
Mtoto ambaye anapata uji wa mbaazi, mtoto anakuwa na
nguvu lakini pia akili yake inakuwa sawasawa na hivyo kuwa na taifa lenye nguvu
kazi inayojielewa.
Utakumbuka zamani soko letu kubwa lilikuwa nchini India,
kwa sasa hali imekuwa tofauti, masoko pekee ambayo tunategemea ni ya ndani,
mimi kama Mwalimu nimeanza kuandika Kitabu lengoni kuhamasisha vijana na jamii
kwa ujumla kuona umuhimu wa zao hilo,” aliongeza.
Kimsingi zao la mbaazi hapa
nchini linazalishwa kwa wingi katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Dodoma
na Manyara. Zao hili lenye faida nyingi kwenye mwili wa binadamu linafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda wa chini kutoka
usawa wa bahari na pia hata sehemu za nyanda za juu nazo zinafaa kulimwa zao
hili.
Ni zao linalostahimili ukame na hili linalifanya
kulimwa hata katika maeneo yanayopata mvua za wastani na yale yanayopata mvua
kwa kiasi kidogo.
Mbaazi hukua vizuri katika maeneo yenye wastani
wa mua wa mm 400-1000 kwa mwaka,katika maeneo yenye mvua zaidi ya mm 1000 kwa
waka hustawi ila ni rahisi kupata ugonjwa wa mnyauko.
Mbaazi hustawi vizuri katika hali ya joto ya
nyuzi 18-30 C. Pia kama hali ya udongo na unyevu ni nzuri zinaweza kukua
vizuri katika hata katika 35 C.
Mbaazi zinastawi katika udongo wowote ambao
hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia
linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo
yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.
Hustawi vizuri katika udongo wenye pH 5-7, Pia pH
4.5 – 8 zinaweza kulimwa
kuna aina kuu tatu za mbaazi, kuna Mbaazi za muda
mrefu: Hizi ni mbaazi ambazo zinawezwa kuvunwa katika misimu zaidi ya miwili.
Huchukua muda mrefu kukua hadi kuvunwa kwa mbaazi
zake.Baada ya mbaazi kuvunwa Mbaazi hukatwa nusu yake na kuruhusu Machipukizi
yake kukua na kuvunwa tena msimu unaofuata na zoezi hili hufanyika ziadi ya
msimu mmoja.Huchukua Siku 180 hadi 270 kupandwa hadi kuvunwa.
pia zipo Mbaazi za Muda wa kati; Hizi hulimwa kwa
msimu mmoja ila huchukua mda wa kati katika kukomaa kwake. huchukua siku 140
hadi 180.
vilevile zipo Mbaazi za muda Mfupi, hizi hulimwa
kwa msimu mmoja na baada ya kuvunwa mimea yake hukatwa na kung’olewa na
kupandwa mbegu mpya msimu unaofuata. mbegu hizi huchukua siku 120 hadi 140.
mpenzi kama unataka kulima zao hili
hakikisha unaandaa shamba lako mapema
kadri utakavyoweza kulima kulingana na aina ya kilimo unachotumia, hakikisha
umeondoa magugu shambani na uchafu mwingine ambao unaweza kuinyima mimea ya
mibaazi kukua vizuri.
Jinsi ya kupanda Mbaazi za Muda
Mirefu; Panda kwa mistari kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 150 kwa
100.(Sentimeta 150 Mstari na mstari na sentimeta 100 Shina hadi shina katika
mstari)
kuhusu Mbaazi za Muda wa Kati; Mbaazi.Panda kwa
mstari nafasi ya sentimeta 100 kwa 60
Mbaazi za Muda Mifupi; Panda kwa
mstari kwa umbali/ nafasi ya sentimeta 90 kwa sentimeta 60
Maaneo ya Pwani ambayo yanarutuba kwa wingi na
joto la kutosha mimea inakuwa kwa kasi na ili upate mavuno bora lazima
uhakikishe mimea yako unaipa nafasi ya kutosha,Hivyo uwe makini na nafasi za mimea
yako unapopanda shambani.
Mara nyingi zao la mbaazi halihitaji matumizi ya
mbolea na samadi. Ijapokuwa Hustawi zaidi katika shamba lenye rutuba ya
kutosha.
Mimea ya mibaazi huitaji kupaliliwa mapema ili
kufanya ikue katika hali ya afya bora na kusaidia kuongeza mavuno yako.
Mbaazi ni mojawapo ya mazao ambayo hayashambuliwi
sana na wadudu japokuwa wapo wadudu ambao kuna maeneo mengine hushambulia kwa
kiasi kikubwa mbaazi nao ni funza wa tumba na wadudu wapekechaji wa mbaazi.
Zuia wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama ATTAKAN-C,Karate au dawa nyingine za
wadudu.
Ugonjwa mkuu unaoshambulia mbaazi ni mnyauko wa
fusaria (fusarium wilt).Ambao husababisha shina la mbaazi kuwa na rangi
nyeusi,ugoro au kahawia. Ugonjwa huu huzuia mfumo wa usafirishaji wa mmea.
Zuia ugonjwa huu kwa kuzungusha mazao shambani
kila baada ya msimu kuisha.Usipande kila msimu mbaazi tuu. Kila msimu badilisha
zao.
Mbaazi zikishakomaa na kuanza kukauka zivunwe
mapema kwa kukatwa matawi yenye mbaazi na kukaushwa zaidi kisha Mbaazi
zitenganishwe kwa mikono au kwa kupigwa hayo matawi taratibu baada
ya kukaushwa sana.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni