Jamii Forum, Doris Mollel Foundation wakubaliana kupeleka ujumbe sahihi wa watoto njiti kwa jamii, lengo ni jamii kufahamu kuwa sababu za kuzaliwa mtoto kabla ya muda wake
Taasisi ya Kiraia ya Jamii Forums pamoja na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wameingia mkataba wa makubaliano wa kupeleka ujumbe sahihi kwa wananchi kuhusiana na watoto wanaoizaliwa kabla ya wakati (njiti).
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi na Mhasisi wa Doris Mollel Foundation Bi.Doris Mollel amesema wao kama taasisi wanafanya kazi kushirikiana na Wizara ya Afya na tayari taarifa sahihi ambazo wanazipeleka katika jamii zimeshapitishwa na kitengo cha elimu ya afya kupitia Wizara ya Afya.
“Tunaamini kupitia Jamii Forums tunaweza kuwafikia watu wengi wanaotumia mitandao ya kijamii na pia sisi ambao ni vijana tunaweza kuwasaidia watoto ambao wanazaliwa kabla ya wakati kwasababu kila mama anaweza kujifungua kabla ya wakati”. Amesema Bi.Doris Mollel.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya kiraia ya Jamii Forums na Waratibu wa mtandao wa Jamii forum Bw.Maxence Melo amesema Jamii Forums inauhakika wa kuwafikia wananchi wasiopungua Milioni 10 hivyo kuingia makubaliano na taasisi ya Doris Mollel Foundation wanaamini watawafikia wananchi wengi na kuelewa kuhusu mtoto kuzaliwa kabla ya wakati (Njiti).
“Mtoto Njiti ilikuwa haifahamiki sana ila kupitia Dorine Molle Foundation imejitahidi kuhakikisha kwamba elimu ya Mtoto njiti inawafikia wengi na sisi tukaona kwamba kwa namna ya kipekee tumeona tuwape ushirikiano hasa kwa mwezi huu wa Mwezi 11 na si kwa muda mfupi bali kwa muda wa takribani mwaka mmoja na kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha kuhusu chanzo sahihi na taarifa sahihi”. Amesema Bw.Melo.
Nae Daktari bingwa wa magojwa ya watoto wachanga Dkt. Augustine Massawe ameshuhudia Asasi mbili za kiraia ya Doris Mollel Foundation pamoja na Jamii Forums wakisaini makubaliano ya ushirikiano wenye lengo la kupaza sauti kwa jamii kufahamu kuhusiana na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani watoto njiti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam .
Aidha Dkt. Massawe amesema kuwa umri mdogo wa kubeba ujauzito na hali duni ya lishe kwa watanzania ni moja ya sababu ya watoto kuzaliwa njiti ambapo inakisiwa kila watoto kumi wanaozaliwa mmoja anakuwa amezaliwa kabla ya muda.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni