Zinazobamba

Picha : TGNP YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI MARA NA SHINYANGA KUWAPA MBINU KUONGEZA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeendesha warsha kwa waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mara na Shinyanga kuhusu uandishi wa habari juu ya nafasi ya vyombo vya habari katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi.

Warsha hiyo itakayodumu kwa muda wa siku tatu iliyoanza leo Alhamis Agosti 13,2020 yanafanyika Mjini Shinyanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari hao wa ngazi ya jamii katika kuandika habari zenye mrengo wa kijinsia hususani suala la ushiriki wa wanawake katika uongozi.

Akizungumza katika Warsha hiyo, Mwezeshaji Dkt. Ananilea Nkya amesema warsha hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo uongozi wa kisiasa kupitia kuhamasisha jamii kuchangia ongezeko la wanawake na wananchi katika michakato ya uchaguzi kama wapiga kura, watia nia wa uchaguzi na wagombea katika nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa unaotelekezwa na TGNP.

Dkt. Nkya ambaye ni Mwanahabari Mkongwe amesema kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari hasa vyombo vya habari ngazi ya jamii katika kuijuza jamii na kuibua mijadala yenye lengo la kubadilisha mitazamo ya jamii juu ya nafasi na ushiriki wa wanawake katika uongozi, ndiyo maana TGNP imeandaa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari.

Dkt. Nkya amebainisha kuwa waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa ya kutumia kalamu kubadilisha mila na desturi ambazo ni kandamizi na zisizohamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na kutilia mkazo mila na desturi zinazohamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi kama wanaume. 

Amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuhamasisha matumizi ya mila chanya na kubadilisha mitizamo ya jamii juu ya nafasi ya mwanamke katika jamii hususani suala zima la uongozi.
Dkt. Ananilea Nkya akizungumza katika warsha kwa waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mara na Shinyanga  kuhusu uandishi wa habari juu ya nafasi ya vyombo vya habari katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi iliyokutanisha waandishi wa habari ngazi ya jamii 40 kutoka mkoa wa Mara na Shinyanga leo Alhamis Agosti 13,2020 katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde & Patrick Mabula -Malunde 1 blog
Dkt. Ananilea Nkya akizungumza katika warsha kwa waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mara na Shinyanga  kuhusu uandishi wa habari juu ya nafasi ya vyombo vya habari katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi. 

Waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mara na Shinyanga  wakiwa katika picha ya pamoja kwenye warsha kuhusu uandishi wa habari juu ya nafasi ya vyombo vya habari katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi.

Picha zote na Kadama Malunde & Patrick Mabula -Malunde 1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako

Hakuna maoni