NEC: Wananchi jitokezi kuhakiki taarifa zenu katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
Wananchi waliojiandikisha katika Daftari la wapiga kura Mwaka 2015 na wale waliojiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari Awamu ya kwanza wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao pindi Daftari litakapowekwa wazi katika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Semistocles Kaijage katika ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa kwa ajili kuweka wazi mabadiliko yaliyojitojeza kwenye Daftari la Awamu ya Pili ya Kupigia kura na kukabidhi nakala kwa wawakilishi wa vyama vya siasa
Jaji Kaijage amesema uboreshaji huo utaanza Aprili 17 na kukamilika Mei 4 mwaka huu kwa nchi nzima ambapo wamegawa katika ruti tatu na kufanyika kwa siku tatu kwa kila mkoa kwa Tanzania bara na Visiwani.
Hata hivyo amesema jumla ya vituo vitakavyotumika awamu hii ni 4006 badala ya 8031 vilivyokuwa vimekubaliwa hapo awali ambapo kwa sasa vituo 3956 vitakuwa Tanzania bara na 50 Zanzibar.

Aidha amesema uboreshaji huo utafanyika katika kila Kata ambapo kutakuwa na Mwandishi Msaidizi na BVR kit Operator ambao watakuwa na orodha ya vituo vyote katika Kata husika na watendaji hao watakuwa na uwezo wa kuboresha taarifa za mpiga kura yeyote.
Aidha amesema wananchi hususani wenye sifa ya kujiandikisha kama wapiga kura wapya wasisubiri kujitokeza siku ya mwisho ya zoezi na hivyo kusababisha msongamano bali wafike vituoni mara tu zoezi litakapowafikia na watuze kadi zao.
Sambamba na hayo Jaji Kaijage amesema NEC haina wataalamu wa Afya ila imenunua vifaa vya kujikinga kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid 19 unaisababishwa na virusi vya corona na tayari wametoa maelekezo kwa watendaji wake kuzingatia miongozo ya wataalamu wa Afya
No comments
Post a Comment