Zinazobamba

TUNDU LISSU AMVURUGA IGP SIRRO,SASA AAMUA KUWA MBOGO KWA WANAOMJADILI,SOMA HAPO KUJUA


TUNDU lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki ni kama ameanza  kukichanganya kichwa cha Mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro baada ya kutaka  mjadala  Lissu Ufungwe mara moja.

Lissu ambaye  alipgwa risasi   na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo akiwa ziarani jijini Mbeya wakati akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo amewaonya wanasiasa kuacha kuuendeleza mjadala wa jambo hilo na waliachie jeshi la polisi lifanye kazi yake.

Mbali na hilo IGP Sirro amewataka wananchi hususani wa mkoa wa Mbeya, kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutii sheria bila shuruti na kwamba, Jeshi la Polisi litahakikisha linawachukulia hatua kali za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.

Aidha Sirro amedai kuwa takwimu za uingizwaji na utumiaji wa dawa za kulevya imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kufanyika kwa operesheni za mara kwa mara zinazofanywa na Jeshi hilo la polisi