Zinazobamba

KASHFA YA USHOGA YATIKISA DAR,MENEJA WA HOTELI MAARUFU ANASWA,SOMA HAPO KUJUA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Meneja Mkuu wa Hoteli ya  Peacok kwa kosa la kuhifadhi watu 12 wanaodaiwa kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja (Ushoga).
Watu hao ni raia wa Afrika Kusini 2, Uganda 1 na  wa hapa nchini wakiwa 9.
Hayo yamebainishwa leo jijini humo na Kamanda wa Kanda hiyo, ACP Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kwa sharia za nchi kuhamasisha ushoga ni kinyume cha utamaduni na Sheria za nchi.
“Kitendo cha kuhamasisha kuingiliana kinyume na maumbile ni kosa la kisheria, vitendo hivyo vya ushoga haviruhusiwi nchini,” amesema ACP Mambosasa.
Aidha ameonya mwananchi yeyote Dar es Salaam atakaye hifadhi watu wa jinsi hiyo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Wakati huo huo Jeshi hilo limefanikiwa kukamata Silaha aina ya SMG, Bastola moja aina ya CZ Magazine mbili, risasi 17, Mabomu aina ya Graned  saba, pikipiki moja aina Ferkon na kuwaua majambazi watano ambao hawakutambuliwa majina. 
Katika hatua nyingine, Kamanda Mambosasa ameeleza kupatikana kwa magari ya wizi, vitu mbalimbali vikiwemo laptop 3, simu 100 na kukamatwa kwa watuhumiwa 9 wa wizi huo.