YASEMEKANA TECNO KUJA NA MFUMO MPYA WA KAMERA, SOMA HAPO KUJUA
Hua tunafahamu kua TECNO huachilia simu zao kubwa ndani ya miezi ya septemba, ikiwemo PHANTOM, lakini sasa ni October na mwaka unaenda kukata, na kwa hisia zangu nahisi mwezi huu watatoa toleo jipya la Phantom. Nafahamu wamechelewesha ila ukiniuliza nitasema ni kwa sababu wanaandaa na kuhahkikisha wanatupa kitu freshi, kizuri na kikali sana kisicho cha kawaida, naweza kusema labda wanaweza kutuweka kwenye hali ya kushikana mashati kutaka kumiliki simu kali kama hiyo itakayotoka.
Vyovyote vile ina litakavyokua iwe ni Phantom 7 au 8, mimi nipo kuzungumzia yale nayotamani yawe kwenye hiyo simu. Tuache kuongea sana na tuzungumzie Camera, nikiulizaz tu ni simu gani itaitwa simu bomba na kali kama camera yake ni kama unapiga picha ya CCTV? Haileti maana.
Ni wakati sasa TECNO waanze kutupatia mfuma wa DUAL CAMERA kwenye simu zetu, na sizungumzii mlichokifaya kwenye Phantom 6, nazungumzia viwango vingine vya juu zaidi vya mfumo wa DUAL CAMERA ambayo zipo kwenye soko la smartphones. Pamoja na hayo niliyozungumza, kuna vitu pia ningependa kuona kwenye huo mfumo wa Dual Camera.
• Uimarishaji kamili wa picha kwenye kamera zote mbili
• Mwongozo wa kuleta chaguzi (more options) zaidi za kupiga picha kwa wapiga picha wa kitaaluma
• zoom ya 2x ya macho
• Uwezo wa kuEdit picha (rekebisha) baada na kabla ya kupiga
(Mfumo wa Dual Camera)
Na mambo mengine zaidi kuweza kutosheleza matumizi ya wapiga picha wachanga na wenye taalumza ya upigaji picha!
Bila kusahau sifa za kuchukua picha za mjongeo (video shoot), ningependa kama TECO wakutufurahisha kama wangeweka “4K shooting mode”
Cha ziada ni kwamba natarajia makubwa na mengi sana kutoka kwenye hili toleo jipya kutoka TECNO, haswa kwenye suala la kamera na mfumo mzima wa utendaji wa simu.