CHADEMA WAMVAA IGP SIRRO WAMTAKA AFUNGE MDOMO HARAKA,SOMA HAPO KUJUA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini ( IGP), Simon Sirro kuacha kutoa vitisho kwa wananchi na wanasiasa kwa kuwataka waache kuzungumzia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), (Tundu Lissu kupigwa risasi 38 mkoani Dodoma kwa kuwa hiyo siyo kazi yake, anaandika Mwandishi wetu.
Chadema wamesema hakuna sheria yoyote inayompa Sirro mamlaka hayo na kwamba anatakiwa kuacha kutoa kauli za kuwanyamazisha.
Chadema wamesema hakuna sheria yoyote inayompa Sirro mamlaka hayo na kwamba anatakiwa kuacha kutoa kauli za kuwanyamazisha.
Kauli hiyo ya Chadema, imetolewa leo na Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya alipozungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho.
Amesema Sirro hana ubavu wa kuzuia watu wakiwamo wanasiasa kuendelea kujadili suala hilo.
“Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki na fursa kwa wananchi kutoa maoni na mawazo yao na kupashana habari pamoja na sheria nyingine na ibara hii ndio msingi, ” amesema Malya.
Aidha, ameeleza kuwa Sirro anaongozwa na sheria kubwa ya jeshi la polisi na huduma saidizi ambayo inatoa maelezo ya nani anaweza kumuamuru, na kuwa na mamlaka ya kuamuru askari wake na siyo raia wa kawaida.
“IGP anyamaze andelee na upelelezi, msisikilize Sirro anachoeleza hamvunji sheria kwa kujadili nani amejaribu kumuua Tundu Lissu, msiingilie upelelezi wao sawa, msiwazuie kufanya upelelezi sawa lakini jadilini,” amesema.