Zinazobamba

ALIYEMUITA RAIS MAGUFULI "KILAZA" MAHAKAMA YAAMUA HIVI,SOMA HAPO KUJUA


Mhasibu wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph, Elizabeth Asenga (40) amehukumiwa kulipa faini ya Sh 5 milioni ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukutwa na hatia katika shitaka la kutuma ujumbe wa kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi, ametoa hukumu hiyo leo Jumanne baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na utetezi uliotolewa na mshtakiwa mwenyewe na kumhukumu mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh 5 milioni ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kukwepa adhabu ya kifungo.
Kesi hiyo namba 317 ya 2016 mshtakiwa huyo alidaiwa kuwa Agosti 6, 2016, aliwasilisha ujumbe wenye mazingira ya kumkashifu Rais Magufuli kwa njia ya WhatsApp kwenye kundi la kijamii liitwalo STJ Staff Social Group.

Mshtakiwa huyo aliandika ujumbe usemao: ‘Godmorning humu. hakuna Rais kilaza kama huyu wetu duniani, angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala lile, picha yake ukiiweka ofisini ni nuksi tupu. Ukiamka asubuhi, ukikutana na picha yake ya kwanza siku inakuwa mkosi mwanzo mwisho.”

Baada ya kusomewa shitaka hilo alikana na alikuwa nje kwa dhamana kwa  kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja wao alisaini hati ya dhamana ya maneno ya Sh 2 milioni.