Zinazobamba

TANZANIA INA AMANI YA GELESHA "ASEMA ASKOFU MKUU,SOMA HA[P KUJUA

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Endtime Harvest (EHC) lenye Makao Makuu Mkoani Dodoma, Dk. Elia Mauza amesema Tanzania haina amani ya kweli badala yake watu wake wana utulivu, anaandika Dany Tibason.
Ametoa kauli hiyo jana wakati wa kongamano la maombi ya kuliombea taifa, viongozi wa kisiasa, serikali, viongozi wa dini pamoja na kuliombea Bara la Afrika.
Kiongozi huyo wa kiroho amesema ambaye pia ni katibu wa umoja wa Madhehebu mkoa wa Dodoma amesema kwamba kuna kila sababu ya kufanya maombi ya kuliombea taifa kwani kwa sasa hakuna amani ya kweli bali kuna utulivu.
Amesema maombi hayo yanayohusisha jumla ya nchi 11 kutoka barani Afrika na mataifa ya ulaya yanalenga kuombea nchi ya Tanzania, nchi za Afrika pamoja na dunia kwa ujumla ili iweze kupatikana kwa amani ya kweli.
“Ili nchi iwe na amani ya kweli ni lazima watu wake wawe na hofu ya kimungu na wafanye kazi kwa kusimamia misingi ya haki, sheria, kanuni pamoja na taratibu za nchi husika badala ya kutumia mabavu au kuongoza kwa kuvunja sheria.
“Tunaweza kuona kwa sasa amani iliyopo nchini ni kubwa kiasi gani lakini matukio yanayotokea ni ya amani kweli wapo watu wanafanya fujo na watu wengine wanavamia na kupiga watu risasi,bado kuna watu ambao wanafanya vitendo vya kiarifu, wala rushwa pamoja na mafisadi.
“Hiyo kama haitoshi wapo watu ambao wanafanya hujuma za wazi wazi kwa viongozi wa kisiasa, serikali, ndani ya viongozi wa Kiimani na makundi ya walionacho na wasiyonacho kwa kutumia vibaya madaraka au mali walizonazo,” alieleza Dk. Mauza.
Hata hivyo Dk. Mauza amesema ili kuendeleza maombi ya Amani ya Tanzania na duniani kote kuna kongamano lingine ambali linaratibiwa na The Global Revival Network litakalofanyika wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Amesema lengo kubwa la kufanya komgamano hilo Kiteto ni kutaka kurejesha amani, upendo na mshikamamo kwa wananchi wa wilaya hiyo kutokana na kuwepo kwa mapigano ya muda mrefu kati ya wafugaji na wakulima.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa mataifa kwa dini ya Kikristo katika kutafuta Amani Duniani, Madh Krishina kutoka India, akiwa katika kongamano la Amani la kuliombea taifa la Tanzania na dunia kwa ujumla, amesema njia pekee ya kupata amani ni kumtanguliza Mungu kwa kila jambo.
Dk. Krishina amesema kuwa wapo baadhi ya viongozi na watawala mbalimbali kutumia majeshi na vyombo vya dola huku wakishindwa kumtanguliza Mungu mbele ili awe kiongozi mkuu katika maamuzi yao.
Kiongozi huyo amesema nchi au bara lolote haliwezi kuendeshwa kwa mabavu au kwa kutegemea mali nyingi za nchi au bara bali ni kujijenga katika misingi ya kuwa na hofu ya kimungu.
“Lazima mjue ili kuwepo na amani ya kweli nilazima watu wakamjua Mungu vizuri ikiwa ni pamoja na kutenda matendo ambayo yatakuwa na haki na sambamba na kuwajali watu wote ambao wanatakiwa kutumiwa,” amesema Dk. Krishina.