Zinazobamba

SERIKALI YA JPM YASUTWA KILA KONA ,HATUA YAKE YA FUNGIA FUNGIA MAGAZETI,SOMA HAPO KUJUA


SIKU moja kupita baada ya Serikali kuchukua hatua dhidi ya gazeti la RAIA MWEMA. kwa lifungia ndani ya muda wa siku 90 kwa kile ilichodai kuwa limetunga nukuu za uongo dhidi ya Rais, Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Facebook.
"Serikali ya CCM ya Awamu ya 5 inaongoza kufungia magazeti kuliko Serikali zote zilizopita. Sababu za Kufungia gazeti la RaiaMwema hazina msingi wowote na ni aibu kubwa. 

Ukosoaji unaofanywa na RaiaMwema ni ukosoaji wenye staha unaopaswa kulindwa kwenye jamii yeyote yenye kuheshimu demokrasia.

Kama hutaki kukosolewa huna sifa ya kuwa Kiongozi wa Umma, tena kwenye Nchi ya wastaarabu Kama Tanzania."



 MBUNGE LEMA NAYE AFUNGUKA

"Raia Mwema limfugiwa kabla kabla #KanunuZa MaudhuiZaUtangazaji hazijaanza kutumika.Zikianza kutumika tofauti yetu na North Korea itakuwa haipo," amesema Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.



Jana Serikali ililifungia Gazeti hilo kwa siku 90 kwa madai kuwa limeandika habari ya kumchafua Rais John Magufuli. Kufungia kwa Raia Mwema inaweka rekodi ya ndani ya siku 10 kufungiwa kwa magazeti mawili kwani tayari wiki iliyopita lilifungiwa gazeti la Mwanahalisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo,Dk Hassan Abbasi kwa vyombo vya habari inasema serikali imefikia hatua kulifungia gazeti la Raia Mwema kutokana kuandiika nukuu ya uongo kwa Rais Magufuli.

Amesema toleo la namba 529  la terehe 27 semptemba hadi Oktoba mwaka ilichapisha habari ya Uchambuzi inayosema “URAIS UTAMSHINDI JOHN MAGUFULI