SAKATA LA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU,MWENDELEZO WA HALI YAKE NI HUU HAPA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SAA chache kupitia baada ya Kupigwa Risasi na watu
wa wasiojulikana,Mkosoaji mkuu wa serikali ya John Magufuli,Tundu lissu leo
mkoani Dodoma alipokuwa ametoka kwenye vikao vya Bunge vinavyoendelea.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema,Freeman Mbowe ,amesema Hali ya Mbunge huyo wa Singida Mashariki hali
yake ni Mbaya sana.
Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani
Bungeni amesema kwa sasa Lissu amepelekwa kwenye chumba cha upasuaji kwenye hospitali
ya rufaa ya Dodoma kwa ajili ya matibabu.
Mbali na Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai kufika
Hospitalini hapo pia waliongazana na Katibu wa Bunge ,Dk Thomas
Kashilila,viongozi wengine wabunge pamoja na ndugu za jamaa za Rais huyo wa
Chama cha Sheria nchini (TLS) huku wakiwa wanalia kwa uchungu baada ya tukio
hilo.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles
Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi
wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo
wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge,
Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa
madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa
na Bunge kwanza.
TUNDU LISSU NI NANI
Tundu Lissu ambaye kwa
sasa amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa ambaye amekuwa akikumbana na kazia ya
kumatwa na kuwekwa ndani hata kufunguliwa kesi za uchozezi mara kwa mara
kutokana na kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi kwa Rais Magufuli na Utawala wake
na kupelekea kufunguliwa kesi zaidi ya nne katika mahakama mbali mbali nchini.
Vitu ambavyo alivyokuwa
akivipinga ni hatua ya kuminya demokrasia pamoja na katazo la vyama vya siasa
kutofanya mikutano ya siasa mpaka 2020 ambalo lilitolewa na Rais Magufuli kwa
hoja ya watu wafanyekazi.
Mbali na hayo,Tundu Lissu
hivi karibuni aliibuka na kufichua tuhuma nzito za kushikiliwa ndege mpya za
Bombardier zilizoshikiliwa nchini Canada kutoka na serikali kuvunja mkataba na
kampuni moja ya ujenzi wa barabara miaka 13 iliyopita na kupelekea kampuni hiyo
kwenda mahakamani kupinga kuvunjiwa mkataba huuo na mahakama kuamulu ndege za
Tanzania kushikiliwa na hadi pale itakapolipa deni la Bilioni 87.
Pia Tundu Lissu pia
kutokana na mvuto wake aliokuwa nao anatajwa uwenda akagombani Urais kupitia
Chadema kwenye uchaguzi wa 2020 kutokana na kukubalika zaidi kwa vijana
kutokana na jina kubwa alilolijenga.