Zinazobamba

KUFUATIA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU,ZITTO KABWE NA MBUNGE SELASINI WAKIMSHA ,SOMA KUJUA

Gari la Tundu Lissu ambalo Risasi limerushiwa

NA KAROLI VINSENT

WAKATI hali ya mkosoaji mkuu wa Serikali ya Rais John Magufuli,Tundu Lissu ikiwa bado ni mbaya kutokana na kupigwa Risasi na watu wasiojulikakana leo mara baada ya Lissu kutoka Bungeni Dodoma kwenye Vikao vya Bunge vinavyoendelea.

Tukio hilo limeanza kulaaniwa vibaya na wanasiasa na watu maarufu huku wakitadharisha nchi kuingia kwenye siasa za mbaya ambazo hazifai katika nchini yenye amani na utulivu.

Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi mkuu wa Cha Act-Wazalendo ameibuka na kuonyesha masikitiko yake kufautiwa tukio hilo la kupigwa risasi Lissu ambaye ni pia ni Mbunge Singida Mashariki .

Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini ametoa masikitikoa yake hayo kupitia Mtandao wake wa kijamii .

"Nchi yetu imefungua ukurasa mpya. Wananchi tusimame imara tusikubali kabisa kuingia kwenye siasa za namna hii. Mola amponye ndugu yetu", ameandika Zitto.

  Kwa upande wake Mbunge wa Rombo ,Joseph Selasini naye akizungumzia tukio hilo la kupigwa risasi kwa Lissu ambaye ni Rais wa chama cha Mawakili nchini (TLS) amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na  gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia.                      

 Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.                       

 "Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema   

 POLISI WANANE.

Akizungumzia Tukio hilo la kupigwa Risasi kwa Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amezungumzia huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kulisaidia jeshi hilo.

Muroto amesema leo Alhamisi kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na wameshafika eneo la tukio nyumbani kwa Lissu.

“Tunaomba mwananchi mwenye taarifa atusaidie. Jeshi la Polisi tumeanza uchunguzi, tumefika eneo la tukio na tunaendelea,” amesema.

Kamanda Muroto amesema taarifa za awali zinaonyesha kuna gari aina ya Nissan lenye rangi nyeupe lilikuwa likimfuatilia Lissu.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amewataka wananchi kuwa watulivu wakisubiri taarifa za Jeshi la Polisi na madaktari wanaoendelea na matibabu ya mbunge huyo, ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema.

     CHADEMA WAFUNGUKA  


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimepokea kwa mshtuko taarifa ya kupigwa risasi mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, amepigwa risasi baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo Alhamisi.

Shambulio hilo limetokea leo mchana nyumbani kwa Lissu, Area D mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

“Chadema tunalaani vikali kitendo hicho na tunafuatilia kwa karibu hali yake,” imesema taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje ya Chadema makao makuu.

Wakati huohuo, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umesema umepokea kwa mshtuko taarifa za kupigwa risasi Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Mratibu wa mtandao huo,  Onesmo ole Ngurumwa katika taarifa amesema wanatoa pole kwa familia ya Lissu, wananchi wa Singida Mashariki, wanachama wa TLS na Watanzania kwa jumla.

Mtandao huo umewahimiza Watanzania wote kumwombea Lissu.

Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge, Job Ndugai amewasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambako Lissu anaendelea na matibabu.                       

Pia, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amefika hospitalini hapo ambako Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, James Charles amesema Lissu yu hai na imara.