MSEMAJI WA SERIKALI AIBUKA NA HILI KWA LISSU,SOMA HAPO KUJUA
Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amefunguka na kusema kuwa hakuna masharti yoyote serikali imeweka ili Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu apatiwe matibabu na kusema wanasubiri maombi ili waweze kugharamia matibabu ya Lissu.
Msemaji wa serikali amesema hayo jana kupitia mtandao wake wa twitter siku moja baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kusema kuwa alipata taarifa kutoka kwa wasaidizi wa Spika wa Bunge kuwa wapo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu kwa masharti ya kuwa mgonjwa lazima apelekwe India, wapate barua ya maombi na kupata ripoti ya madaktari jambo ambalo Mbowe anasema alilikataa na kusema hawezi kufanya hivyo.
Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo ndipo Msemaji wa Serikali ameibuka na kusema kuwa hakuna masharti yoyote ambayo wameyaweka na kusema serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu na kuwa wao wanasubiri barua kujua gharama za matibabu.
"Hakuna sharti lolote, tunasisitiza tena na bado tunasubiri, leteni barua rasmi tujue gharama na itifaki nyingine za tiba. Tutagharamia" alisema Dkt. Abbas
Aidha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu aliendelea pia kufafanua jambo hilo kuwa Mbunge Tundu Lissu aliondolewa kwenye utaratibu wa serikali alipopelekwa nchini Kenya hivyo anadai ili serikali iweze kuingia katika gharama za kulipia matibabu lazima wapate ridhaa ya familia.
"Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu wa Serikali alipopelekwa NRB. Sasa gharama/tiba zaid yahitajika. Serikali inaingiaje bila ridhaa ya familia? Mgonjwa ni Mbunge, anahitaji matibabu zaidi. Lakini kwa kuwa sasa yupo nje ya utaratibu wa Serikali, Serikali kushiriki ni lazima yawepo maombi" alisisitiza Ummy Mwalimu