Zinazobamba

MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAONGEZEKA MARA DUFU,SOMA HAPO KUJUA



Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE Mary Kinabo akitoa taarifa ya yeliyojiri kwenye soko la hisa kwa wiki iliyoishia Septemba 22/ 2017 mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam 

KIWANGO cha mauzo  ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 5.4 wiki iliyopita hadi kufikia shilingi bilioni 53.5 mnamo September 22 mwaka huu .

Kuongezeka kwa mauzo ya hisa hizo kumetokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtaji katika kampuni ya Kenya Airways kwa asilimia 20 pamoja na uchumi super market kwa asilimia 12.5pamoja benki ya kibiashara ya Kenya kuongezeka kwa asilimia 9.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Ofisa Masoko  Mwandamizi wa DSE, Mary kinabo amesema kuwa ukubwa wamtaji wa kampuni zandani umeongezeka kutoka shilingi milioni 27 hadi kufikia shilingi trioni 9.5

‘’Makapuni yaliyo ongoza wiki hii katika mauzo ya hisa nipamoja na Benki ya biashara ya CRDB ,DCB Pamoja na Soko lahisa la Dar es salaam’’ amesema kinabo.

Aidha amesema kuwa wakati mauzo ya hisa ya  kiongezeka kutoka bilioni 5.4hadi kufikia shilingi trioni9.5 mauzo ya hati fungani hadi kufikia September mwaka huu yameongezeka kutoka bilioni 22 hadi kufikia bilioni 36.
Amesema kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 30 kutoka pointi 2,098 hadi pointi 2,128 kutokana na kupanda kwa bei za hisa kwenye kampuni ya Kenya Airways, Uchumi Supermarket Ltd na Kenya Commercial Bank.

Hata hivyo Kinabo amebainisha kuwa kiashiria cha kampuni za ndani TSI kimepanda kwa pointi 11 kutoka 3.704 hadi pointi 3,715 huku kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepanda kwa pointi 26 kutoka pointi 5052 hadi pointi 5078.

Ameeleza kwamba kiashiria cha huduma za kibenki na fedha (BI) wiki hii imepungua kwa pointi 2 kutoka pointi 2,520 hadi pointi 2,518 na kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,475.

Akizungumzia juu ya hati fungani amesema mauzo yake katika wiki iliyoishia Septemba 22 mwaka huu yalikuwa sh.bilioni 36 kutoka sh.bilioni 22 wiki iliyopita Septemba 15.

Aidha amebainisha kuwa mauzo hayo yalitokana na hati fungani kumi nan ne (14) za serikali zenye jumla ya thamani y ash.bilioni 40 kwa jumla ya gharama ya sh.bilioni 36.