Zinazobamba

KAMPUNI YA SIMU YA ITEL YASHEHEREKEA MIAKA 10,YAJA NA KITU BORA,SOMA HAPO KUJUA

KAMPUNI ya Simu ya Mkononi ya Kijanja ya ITEL Mobile leo imesheherekea miaka 10 ya kuanzishwa kwake huku itel ikiwa ni moja ya kampuni vinara kwa ubora Barani Afrika.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais wa Itel Leslie Ding, amesema katika kipindi cha miaka 10 itel imeonesha nguvu ya mabadiliko tangu kuingia kwenye soko la Afrika kwa mwaka huu wa 2017.

“Hii ni kutokana nan a baada ya kuanzishwa kwa timu ya watu wenye ujuzi na moyo wa kufanya kazi. Miaka 10 sasa, itel imekua na imeenea Zaidi ya nchi 45 duniani kote. Tunaamini kuwa tuna timu imara ambayo hata mafanikio ya miaka 10 iliyopita ni kutokana na juhudi kubwa iliyofanywa na timu hii,” amesema Ding.

Aidha ameongeza kuwa katika kipindi hicho itel mobile imekuwa na mabadiliko chanya ya bidhaa kutokana na kufuata matakwa ya wateja wake.

Ding ameongeza kuwa kampuni hiyo kwa sasa inapendwa na watu wengi na inamvuto kutokana na bidhaa zao kuboreshwa zaidi kwa ubunifu mkubwa ambapo wameweza kuongeza wateja mara mbili zaidi barani Afrika na kwamba hadi sasa wameweza kuuza simu milioni 100.

Amesema pia mafanikio hayo yamechangiwa na kushirikiana na mastaa wan chi za Afrika kama mabalozi wa kampuni yao na kwamba wamekuwa kiungo muhimu katika kuleta ufahamu na uelewa kuhusu kampuni hiyo ambayo ni miongoni mwa kampuni tatu bora barani Afrika.

Aliongeza kuwa wanaposherehekea miaka 10 wanatarajia nguvu yao ya mabadiliko itakuwa kubwa zaidi na wanaendelea kuliimarisha bara la Afrika kwa kutoa bidhaa bora zaidi za mawasiliano.

Naye Balozi wa Itel nchini Irene Uwoya ameipongeza kampuni hiyo kwa ubora wake ulioifanya kuwa miongoni mwa kampuni tatu bora za barani Afriaka.
Kwa upande mwingine Itel Mobile imezindua simu mpya za kisasa ambazo ni itel S12 na S32.

Akizungumzia simu hizo Ofisa Masoko  wa Itel Saiphon Asajile alisema simu hizo ni bora na zina kamera mbili za kuweza kupigia selif mbili za picha.

Pia katika hafla hiyo kampuni hiyo imetoa tuzo kwa washirika ambao wameweza kufanya vizuri katika biashara na kuchangia mafanikio ya kampuni.

HABARI ZAIDI SOMA HAPO TENA CHINI


IMG_5477Makamu wa Rais wa Itel Mobile Bw.Leslie Ding akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.
IMG_5498Balozi wa Itel Mobile,Irene Uwoya akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.
………………………………
Kampuni ya Simu ya Itel Mobile imetimiza madhamisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku ikiendelea kufanya vizuri katika soko la mauzo ya Simu na kuwa kinara kwa ubora wa bidhaa zake barani Afrika na nje ya Afrika.
IMG_5459Miaka 10 iliyopita Itel Mobile ilizindua mpango wa kumwezesha kila mmoja kuwa na simu bora kwa ajili ya mawasiliano ya uhakika,katika kipindi hicho chote tumepitia katika kipindi kigumu katika Nyanja za kiuchumi na kisiasa lakini tumeweza kufanikiwa kutimiza mlongo mmoja kwa uthabiti mkubwa.
Itel Mobile iliingia kwenye soko la Afrika mwaka 2007 na baada ya kuanzishwa kwa timu ya watu wenye ujuzi na moyo wa kufanya kazi na mpaka sasa miaka 10 kampuni hii imekuwa na kuweza kuenea zaidi ya nchi 45 Duniani kote.
IMG_5465
Ndani ya miaka 10 Itel Mobile imekuwa na mabadiliko makubwa chanya ya bidhaa kutokana na kufuatwa matakwa ya wateja wake hivyo imepelekea kupendwa na kuleta mvuto kutokana na kuboreshwa kwa bidhaa hizo kwa ubunifu mkubwa.
”Tumeweza kuongeza idadi ya wateja mara mbili zaidi barani Afrika na pia shukrani zetu za dhati ziende kwa wateja wetu pamoja na mashabiki wote wa Itel na mpaka sasa tumeuza jumla ya simu milioni 100’alisema Makamu Rais
IMG_5480Aidha nguvu kubwa yetu inatokana na bidhaa zetu zilivyo bora pamoja na timu ya wafanyakazi wetu ambao kila mmoja amekuwa akijituma kutokana na nafasi yake na pia ubora na mvuto wa bidhaa unatokana na mapendekezo ya watumiaji wetu na huduma za matengenezo baada ya mauzo na warantii ya miezi 12 kwa bidhaa zetu zote.
IMG_5486Hata hivyo tumekuwa na ushirikiano na mastaa wa nchi za Afrikia kama mabalozi wa kampuni yetu na wamekuwa kiungo muhimu katika kuleta ufahamu na uelewa kuhusu kampuni ya Itel ambapo imekuwa kampuni 3 bora barani Afrika.
Na kwa kuonesha upendo wetu Afrika tumekuwa tukifanya matendo ya ukarimu kwa jamii na kujitolea kutembelea baadhi ya shule na vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.
Itel Mobile Tanzania kwa kushirikiana na balozi wa kampuni mwaka huu peke mpaka sasa tumewasaidia katika mahitaji muhimu zaidi ya watoto 400 wanaotoka mazingira magumu wakiwemo yatima na tunaendelea kuunga mkono jitahidi za kusaidia jamii.

IMG_5517Tunaposherekea miaka 10 tunatarajia kuleta mabadiliko makubwa zaidi ili kuimarisha bara la Afrika kwa kutoa bidhaa bora za mawasiliano na leo tunazindua simu mpya ambazo ni za kisas zaidi yaani Itel S12 na S32 na zina ubora kutokana na kuwa kila  simu simu ina kamera mbili za mbele pia mwonekano mzuri na kusaidia kuchukua selfie ya kundi ambayo ina uwezo wa kuchukua watu wengi zaidi pia zina Fingerprint ‘alama za vidole’.