Zinazobamba

KAMATAKAMATA YA WABUNGE WA UPINZANI YAANZA TENA,MBUNGE HUYU AKAMATWA JIONI HII,SOMA HAPO KUJUA

Hali ya kukamatwa kamatwa ya Wabunge wa Upinzani Nchini Hususani Chadema ilikuwa imetulia baada macho na masikio ya wengi kuelekezwa kwenye kumtibu Mbunge wa Singida masharki ,Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwezi huu mjini Dodoma,
 Hali  ya kukamatwa kamatwa ni kama imeanza tena ndivyo naweza kusema baada,Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema) kukamatwa na polisi leo Jumapili jioni baada ya kushushwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Iringa Mjini (Bavicha), Leonce Marto alikiambia Chanzo cha Fullhabari.blog, kuwa mbunge huyo alikamatwa saa 11:24 jioni na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) aliyekuwa ameambatana na polisi wengine kisha wakampeleka ofisi za mkoa za jeshi hilo.
“Kutoka Mlandege mpaka ofisini kwa kamanda wa mkoa amebadilishwa kwenye magari matatu. Tunahisi atakuwa anasafirishwa ingawa bado anahojiwa. Yupo ndani, sisi tunaendelea kumsubiri nje,” amesema Marto.
Mwenyekiti huyo alizungumza na Chanzo changu kupitia simu ya mbunge huyo na kubainisha kwamba mpaka wakati huo (saa 12:30 jioni) jeshi hilo halikubainisha sababu za kumshikilia Msigwa.
“Alikuwa na kibali cha kufanya mkutano katika kata tatu kuanzia leo Jumapili mpaka Jumanne. Alianza kuzungumza saa tisa alasiri ilipofika saa 11:24 jioni, RCO akiwa na polisi wengi wakamshusha jukwaani na kuondoka naye,” alisema Marto bila kufafanua sababu za kukamatwa.