HATIMAYE SASA TUNDU LISSU AANZA KUTIKISA ANGA ZA KIMATAIFA,APATA SHAVU KUBWA,SOMA HAPO KUJUA
HATIMAYE nyota ya Mbunge wa Singida
Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS),Tundu Lissu imeanza kung’aa katika anga za kimataifa ndivyo naweza kusema ,baada ya
Gwiji huyo wa sheria nchini kupata Mwaliko kwenye mkubwa wa sheria Duniani.Anaadika
Karoli Vinsent Endelea nayo.
Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema amepata Mwaliko katika Mkutano wa Mawikili
Bingwa wa Sheria Nchini Marekani.
Mkutano hao unatarajiwa kuhudhuliwa na mawakili
Bingwa kutoka nchini tofauti Duniani utarajia kufanyika Jiji la Washington Dc
siku ya Ijumaa ya tarehe 15/09/2017.
Lissu ambaye kwa sasa ametajwa kuwa ndio mkosoaji
mkubwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kutokana na
serikali hiyo kutuhumiwa kuminya Uhuru wa Kujieleza pamoja kukandamiza vyama vya upinzani ,baada ya Rais Magufuli kukataza vyama vya siasa visifanye kampeni mpaka 2020 kinyume na katiba inavyosema.
Licha ya Katazo hili ndani ya utawala wake
kumeshuhudiwa kuongezeka kwa kasi ya kukamatwa kwa viongozi wa Chadema pamoja na
wabunge wao,kwa mujibu wa Chama hicho cha Upinzani wanasema mpaka sasa tangia
Magufuli aingie madarakani ni teyari viongozi 400 wa chadema wamekamatwa na
Polisi .
Katika Mkutano huo, Lissu anatajwa kuwa ni Mwafrika wa kwanza kuhudhulia .sababu inayotajwa kwa
Gwiji huyo wa sheria kupewa mwaliko kwenye mkutano huo kunatokana na Umahiri
wake wa sheria pamoja na kujitokeza kuwatetea wanyonge kupitia sheria.