Zinazobamba

CHAMA CHA ADC CHATOA NENO TUKIO LA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU,SOMA HAPO KUJUA



Pichani ni (katikati) ni  Doyo Hassan Doyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
NA KAROLI VINSENT
CHAMA cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimelaani tukio la kushambuliwa kwa kupigwa Risasi ,Rais wa Chama cha Mwakili nchi (TLS)Tundu Lissu ambalo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita mkoaniDodoma,huku Chama hicho kikilitaka jeshi la polisi kuchunguza na kuwakamata watu wote waliofanya kitendo hicho.

Pia Chama hicho kimevitaka vyombo mbali mbali vya ulinzi nchini kuongeza nguvu kwenye ulinzi wa raia na mali zao ,kutokana kukithiri kwa vitendo vya uvunjifu wa amani nchini ikiwemo
kutekwa kwa viongozi wa siasa pamoja kuuliwa kwa wananchi wasio na hatia.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Katibu mkuu wa (ADC)Doyo Hassani Doyo amesema Chama hicho kimesikitishwa kwa kitendo alichofanyiwa Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida mashariki huku wakisema matukio hayo yanajenga picha mbaya ndani ya nchi.

Amesema kwa sasa nchini matukio kama yalioyomkuta Tundu lissu yamekuwa yakitokea mara kwa mara jambo analodai linaita doa taifa.
"Chama chetu kimebaini matukio kama  hili la Lissu sio geni  katika siku za karibuni kwani tunayokumbukumbu  ya kutekwa kwa Ulimboka,Ben Saa Nane,Kibanda na wengine "Amesema Doyo.

Doyo amesema kuwa Chama cha ADC kimetafakari kwa kina juu ya matukio hayo ambayo chama hicho kimedai yanaendelea kutokea mara kwa mara nchini huku kikitoa ushauri wa kwa Vyombo vya ulinzi pamoja na serikali kutoyachukulia matukio hayo kwa namna ya mazoea.

"ADC tunashauri serikali hasa vyombo vya ulinzi na  Usalama  visichukulie vitendo vya uharifu kwa mazoea bali kuna kila sababu ya kuunda kikosi maalum ambacho kitakuwa na watu wenye weredi wa hali ya juu katika kukabiliana na matukio ya namna hii''Amesema Doyo.

Katika hatua nyingine Chama hicho  kimeitaka serikali kuhakikisha wanakomesha vitendo vya rushwa ambavyo vimekithiri nchini huku chama hicho kimesema vitendo vya rushwa vinakwamisha juhudi za wananchi kujiletea maendeleo.