CHADEMA YAITEGA SERIKALI KUHUSU OPARESHENI UKUTA,SOMA HAPO KUJUA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetonesha kidonda kilichopona baada ya kusisitiza kwamba bado kina dhamira ya kufanya maandamano kwa nchi nzima waliyoyapa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA), anaandika Victoria Chance.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Chadema, Vicent Mashinji amesema, suala la Ukuta ni endelevu na siyo kufanya mikutano na mandamano pekee.
Amesema wananchi wengi wanapenda tudai katiba yetu kwa nguvu, lakini sisi kama chama tuna njia ambazo tumeziandaa.
Njia ya kwanza wanahoja binafsi ambayo italezea maboresho ya tume ya uchaguzi ambayo itawasilishwa bungeni.
“Pia tunatumia njia za kidiplomasia na kidemokrasia kuhakikisha kwamba suala hili linafika mwisho wake na endapo njia hizi hazitafikia lengo tutawaomba wananchi wachukue uongozi katika suala hilo,’’ amesema