Zinazobamba

Burundi: Wanawake waandamana kupinga ripoti ya Umoja wa Mataifa

Maelfu ya wanawake nchini Burundi waandamana kupinga ripoti ya Umoja wa Mataifa inayotuhumu serikali ya Bujumbura

Maelfu ya wanawake nchini Burundi wameandamana Jumamosi  kupinga ripoti ya Umoja wa Mataifa ilitolewa Jumatatu ililopita.

Jumatatu wajumbe wa Umoa wa Mataifa waliofanya uchunguzi na kutoa ripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi  waliitaka mahakama ya kimataifa ya ICC kufanya  uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa  imewatuhumu viongozi wa ngazi za juu nchini humo kuhusikka katika vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Maelfu ya wanawake mjini Buumbura  waliandamana kupinga ripoti hiyo wakidai kuwa lengo la ripoti hiyo ni kuchafua serikali na taifa zima la Burundi.